Wednesday, 9 September 2026
Kenyan Digest

Mvulana wa miaka 16 kuaga dunia na wawili kupokea matibabu

1 min read
Published 23 January 2019

Mvulana wa miaka 16 kuaga dunia na wawili kupokea matibabu

Kifo hakibishi hodi hivyo ndivyo waswahili walivyo sema.

Mvulana wa miaka 16 aliaga dunia, na wengine wawili kupelekwa hospitali kwa matibabu katika hospitali ya kimeshenari ya St. Peters Mumias.

Huku familia zaidi ya hamsini kuachwa bila makao baada ya mzozo kuzuka baina ya wenyeji vijiji vya malomba na etete kwenye mpaka wa kaunti ya Busia na Kakamega.

Inadaiwa mzozo huo uliibuka baada ya vijana kutoka kijiji cha Etete kaunti ya Kakakmega kuzuru kijiji jirani cha Malomba kutafuta wasichana majira ya usiku  kabla ya kufurushwa na wenyeji wa kijiji cha Malomba wakidhani ni wezi wa mifugo wamewasili kuwavamia.

Huku wakimpiga kijana huyo hadi wakamuua, na kuwajeruhi vijana kadhaa.

Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Butula, Winston Murugi alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa wenyeji wa kijiji cha Utete waliamua kulipiza kisasi.

Kwa kuteketeza nyumba zaidi ya hamsini katika kijiji cha malomba, eneo bungela Butala.

Lakini swali ni nani atawasaidia wana kijiji hao wasiokuwa na mbele wala nyuma.

Murugi alisema kuwa usalama umeimarishwa katika mpaka wa kaunti ya Busia na Kakamega ili kuzuia maafa na uharibifu wa mali.