Grace Wambui Odogo ni mwanamke ambaye wananchi wengi walimpongeza na kutaka kumjua kwa kitendo alicho kifanya katika shambuliziya la DusitD2.
Wambui alijitolea kupika chai na kuwapelekea askari waliokuwa wameshika usukani katika eneo hilo.
“Nilijua shambulizi hilo saa kumi baada ya jirani yangu kutuambia tuwashe televisheni, kisha nikaenda kanisani kwa maana napenda sana mambo ya Mungu.
Baada ya kutoka kanisa niliweza kufikiria nitawasaidia polisi kivipi na nini ndio nikaanza kupika chai,”Grace alisema.
Grace anayeishi karibu na kituo cha polisi cha kileleshwa, aliweza kumpigia OCPD wa kituo hicho simu ili aweze kumueleza atakapo pikia chai na chenye anaweza.
OCPD alimueleza vile atafanya kisha akampeleka kuekea polisi chai.
Aliweza kuwatumikia polisi hao usiku kucha pia siku iliyofuata kisha akawaandalia chakula.
“Nilipika wali, ugali, nyama na mboga, na kuwaletea tena nilikuwa katika eneo hilo kwa siku mbili, nahudumu katika kanisa la Holy trinity,”Alisema Wambui.
Alisema kuwa penye nia kuna njia, Grace hakupewa pesa na mtu yeyote bali aliweza kutumia pesa zake mwenyewe ili kuwahudumia polisi hao.
Mnamo mwaka wa 2007, Grace aliathirika kibiashara, kwa sababu ya vurugu iliozuka baada ya uchaguzi, kwa madai ya kwamba ni mkikuyu ilhali yeye sio wa kabila ya upande wa Nyanza.
Licha ya kuwa ameolewa upande huo wa Nyanza.
“Nilikuwa nafanya kazi ya biashara kisumu, na pia nimeolewa Nyanza, siku moja tarehe 28 Januari watu walio pitisha kiwango waliingia kwa biashara yangu wakabeba vitu na kisha wakachoma biashara hiyo kitendo kilicho nifanya nitoke Kisumu nije kuishi Nairobi.” Grace alielezea.
Baada ya kuhama, Grace aliweza kumpoteza mamake mwaka wa 2012 tarehe 18 mwezi wa Juni aliyekuwa anaugua ugonjwa wa saratani.
Muda haukupita sana mumewe aliugua saratani,k isukari na ugonjwa wa shinikizo la damu na akaaga dunia mwaka wa 2017.
“Nina watoto wawili mmoja miaka 28 na yule mwingine miaka 27, mmoja ni msichana na mwingine mvulana.
Wakati huo wa vurugu, watoto wangu walikuwa tayari shuleni kwa sababu walikuwa wanasomea Uganda, kwa hivyo hawakuathirika sana,”Alisema Grace.
Grace ambaye alipongezwa na wananchi, alisema kuwa alikuwa mjasiri na hakuenda kumuona mshauri baada ya hayo yote kutendeka. Aliongezea kuwa Mungu anaweza kupa nguvu na ujasiri wa kupitia chochote maishani.



