Connect with us

General News

Mwanaume kuuwawa na wanawe baada ya kugombana juu ya ngono

Published

on


Mwanamume mmoja jumatatu usiku aliweza kukatwa na wanawe wawili hadi kuachwa hali mahututi baada ya kubishana na mkewe juu ya masuala ya ndani ya kifamilia.

Inasemekana kuwa walitofautiana na mkewe kabla ya wanawe kumvamia na panga.

Mzee wa kijiji hicho alisema kuwa Khalabai aliweza kuenda nyumba kwake saa 9 usiku akiwa amelewa chakari ambapo alianza kudai haki yake ya ndoa.

Alisema kuwa mwanamke huyo alipiga nduru ili aweze kusaidiwa, ndipo mmoja wa vijana hao alienda kuangalia ama kuchunguza nini kilicho kuwa kinaendelea.

wanakijiji wa sindai kaunti ya bungoma

 

Simiyu alisema kuwa wanandoa hao walikuwa waki lala katika vitanda tofauti.

“Mmoja wa vijana hao aliweza kuuvunja mlango na kumpata mamake akiwa anapiga nduru akisema kuwa babayao alikuwa anataka kumbaka.

Kijana huyo alirudi na kisha akarudi na kakake ambapo walianza kumchapa babayao hadi akapoteza fahamu,”Simiyu alisema.

Patrick alipatwa na majeraha mabaya ya kichwa na mguu ambayo alikuwa amekatwa na panga na wanawe hao wawili.

Vijana hao walimuacha mzee huyo pekeyake chumbani katika hali maututi karibu kuchungulia kaburi. Asubuhi yake walimpata akiwa katika hali mbaya na kumpeleka hospitalini.

Walipo tangaziwa alikuwa tayari amefariki kabla ya kufika hospitali.

Wanakijiji walitaka kumuua mwanamke huyo na vijana wake wawili lakini polisi kutoka kituo cha polisi cha kimilili waliwakataza wanakijiji hao waliokuwa na hasira kupindukia.

Mwanamke huyo na kijana mmoja walikamatwa na polisi na mmoja kutoroka. Lakini wanavyo sema mkono wa sheria ni mrefu.

th

Kijana huyo atatoroka hadi lini na atawakimbia polisi hadi wapi na lini? K wa maana wanamtafuta kwa hali yoyote.

Simiyu aliwauliza wanakijii hicho kutafuta namna nyingine ya kutatua matatizo ya ndani ya familia. Pia aliuliza watoto wasichangie upande mmoja wa wazazi wao katika migogoro ya wazazi wao.

Polisi walisema wawili hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi.

 





Source link

Comments

comments

Facebook

Trending