Connect with us

General News

Mziki si mashindano alinifunza mwenzangu Oliver Mtukudzi

Published

on


Mwimbaji wa nyimbo za Afro-fusion Suzzana Owiyo, alisema mwimbaji wa Zibambwe mwendazake Oliver alimfunza hekima ambayo anatumia katika uimbaji wake.

“Nilimpata Mtukudzi kwenye studio,nilikuwa naenda kufanya mahijiano pia, Oliver alikuwa amekuja kutembea Kenya,” Suzanna alisema.

Kupiga gitaa kwake Suzzana ndiko kulimsaidia kulimvutia tahadhari za Mtukudzi.

Msanii wa zimbabwe mwendazake Oliver Mtukudzi

Tangu kupatana mara ya kwanza, wawili hao walijuana zaidi na pia kufanya kazi pamoja licha ya kupatana mara ya kwanza.

“Nilimshitikisha katika albamu yangu yaambayo inaitwa ‘my roots’.Na amekuwa mshauri wangu na pia kusoma mengi kutoka kwa kila mmoja wetu.

“mkiwa marafiki katika tarabu za mziki,kuna mengi ambayo mtasoma kutoka kwa kila mmoja.” Aliongezea Suzanna.

Pia Suzanna aliweza kusema kuwa mwanamziki huyo alikuwa myeyekevu licha ya kujulikana duniani, pia alisema Mtukudzi alimfunza kuwa mziki si mashindano bali mziki unapaswa kuleta watu pamoja.

Soma: My mom, a staunch Christian was against me singing secular songs – Moh Nanah

Oliver alikuwa na shauku na nyimbo za kiafrika, na madhumuni yake yalikuwa kupea watu matumaini wasiokuwa na matumaini na kuponya wenye mioyo yenye iliovunjika.

Suzanna akizungumza na gazetti la the Star, alisema kuwa aliposafiri kuenda Zimbambwe, Mtukudzi alikuwa ameenda kuwasaidia na kukuza vipaji vya vijana ambao hawakuwa wamejulikana.

“Nilikuwa napenda sana vile mwendazake Mtukudzi alivyokuwa anaishi na alihakikisha mziki wake uliwafikia wengi licha ya lugha alioitumia kuwafikia mashabiki wake,” alisema Suzanna.

Suzanna alikuwa anatembelea kituo chake cha sanaa na alitimiza alichokitoa na kuwasaidia wasanii wanaochipuka.

Mwalimu kuanguka na kuaga dunia kwa hali isiyojulikana

Mtukudzi aliweza kutoa albamu 67 zilizowapendeza watu duniani kwote. Alifariki jumatano katika kliniki cha Avenues  clinic katika eneo la Harare.

Mtukudzi alifariki akiwa na miaka 66,alikuwa anaugua ugonjwa wa kisukari kwa miaka mingi.

Read more

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending