NCIC yashtakiwa kwa kupiga marufuku ‘Hatupangwingwi’
NA RICHARD MUNGUTI
MAWAKILI Felix Kiprono na Vincent Kiprono wamewasilisha kesi kupinga marufuku ya matumizi ya “Hatupangwingwi” na “watajua hawajui.”
Tume ya Uwiano na Utangamano Nchini (NCIC) ilipiga marufuku maneno hayo ikisema yanapalilia chuki.
Mrengo wa Naibu Rais Dkt William Ruto unadai NCIC inatumiwa na serikali kuhujumu kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.



