Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Ngirici amteua mhasibu kuwa mgombea mwenza – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 16 May 2022

Ngirici amteua mhasibu kuwa mgombea mwenza

NA GEORGE MUNENE

MWAKILISHI wa Kike kaunti ya Kirinyaga Wangui Ngirici amemteua aliyekuwa naibu kamishna wa Tume ya Ukusanyaji Ushuru Kenya (KRA) Eliud Wanjao kuwa mgombea mwenza wake.

Bi Wangui anayegombea kiti cha ugavana kaunti ya Kirinyaga alisema kwamba Wanjao, ambaye ni mhasibu ana tajriba pana katika masuala ya usimamizi.

Alisisitiza kuwa watabadilisha Kirinyaga iwapo watachaguliwa uchaguzini.


About the author