Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Rice kuwa nahodha mpya wa West Ham baada ya Noble kustaafu mwishoni mwa msimu huu wa 2021-22 – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 1 January 2022

Rice kuwa nahodha mpya wa West Ham baada ya Noble kustaafu mwishoni mwa msimu huu wa 2021-22

Rice kuwa nahodha mpya wa West Ham baada ya Noble kustaafu mwishoni mwa msimu huu wa 2021-22

Na MASHIRIKA

KOCHA David Moyes wa West Ham United amesema azma yake ni kumfanya kiungo raia wa Uingereza, Declan Rice kuwa mhimili mkuu wa kikosi chake.

Rice, 22, atasakata mechi yake ya 150 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) atakapoongoza West Ham kuvaana na Crystal Palace katika uwanja wa Selhurst Park mnamo Disemba 1, 2022.

“Msimu huu, Rice ameimarisha matokeo aliyoonyesha katika fainali za Euro 2020. Amekuwa kivutio cha vikosi vingi vya haiba kubwa Uingereza na bara Ulaya. Lakini mkataba kati yake nasi unaendelea hadi 2024 na atakuwa huru kuongeza mwaka mmoja zaidi kwenye kandarasi hiyo,” akasema Moyes.

Kwa mujibu wa Moyes, Rice ndiye atapokezwa unahodha wa West Ham baada ya kigogo Mark Noble kustaafu mwishoni mwa kampeni za muhula huu wa 2021-22.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO


About the author