Wednesday, 9 September 2026
Kenyan Digest

Tracy Wanjiru aelezea alivyonusurika kifo katika shambulizi la Westgate na DusitD2

3 min read
Published 22 January 2019

Baada ya shambulizi la westgate kumaliza miaka mitano, magaidi wa Alshaabab hawakulaza damu bali waliweza kuwa na mipango ambayo watashambulia tena maduka ya ununuzi yanayokuwa na maelfu ya watu.

Westgate ilishambuliwa 21 Septemba 2013 ambapo zaidi ya watu hamsini walipoteza maisha na wengine kupata majeraha mabaya siku hiyo.

Katika shambulio hilo, Tracy Wanjiru almaarufu (Shiro) alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya duka hilo magaidi walipo shambulia.

Polisi wakishika usukani eneo la westgate

Tracy ambaye alikuwa na uja uzito wa miezi sita, hakuwa ameenda kutembea, wala kujivinjari bali alikuwa kazini akifanya kazi yake ya kila siku kama kawaida.

Alikuwa akifanya kazi katika kampuni la basic intimates wakati magaidi hao walipo shambulia.

“Katika shambulio la Westgate nilikuwa natoka lakini sikua naenda nikae sana, hapo ndipo nilisikia mlipiko na milio ya risasi, sikupatana na magaidi ana kwa ana bali nilikimbia nje nikaenda kukaa huko baada ya dakika kumi ndio nilipojua ni shambulizi, nashukuru Mungu nilinusurika, wenzangu wenye tulikuwa twafanya kwazi na wao hawakufa lakini walipata majeraha,”Tracy alisema.

Katika shambulio hilo aliingiwa na uoga alidhani Mungu alimlinda kwa sababu alikuwa na ujauzito, hapo ndipo tracy alijua mungu ana mpango mkubwa katika maisha yake.

Tracy wairimu(shiro)aliyenusurika katika shambulizi la Westgate2013 na shambulizui la DusitD2

Baada ya shambulizi tracy aliweza kuendelea na kazi alafu baadaye akaenda kujifungua hapo ndipo aliacha kufanya kazi katika kampuni ya basic intimates.

Baada ya shambulio hilo hakuweza kwenda mshauri lakini alikuwa anaenda hospitali tu kama kawaida.

Katika shambulio la DusitD2 wiki iliyopita, Tracy Wanjiru alikuwa meneja wa saluni ya Amadiva, magaidi walipovamia.

“Nilikuwa nimekaa hapo kazini baada ya maakuli ya mchana ndipo nilisikia mlipuko baadaye nikaona kipande cha mguu wa mtu nilishtuka muda usiokuwa mrefu nilianza kusikia milio ya marisasi, nilikimbia nikaenda saluni nakaambia wenzangu kuwa kuna shambulizi lakini hawakuchukulia ni jambo la maana, tulianza kukimbia na kuchanganyikiwa,”alisema Tracy.

Tracy alijificha katika jumba moja ya saluni (Massage room) walipoanza kutawanyika aliweza kumpigia mamake na kumjulisha hali ilivyo katika maeneo hayo,katika nyumba hiyo walikuwa wanne.

Watu wakitolewa katika maenea ya DusitD2

Mmoja wa mteja wa Tracy aliweza kumuomba simu na kumpigia mamake ili pia yeye kumjulisha hali ilivyo, walipokuwa katika chumba hicho, Tracy na wenzake waliweza kuzima stima na pia kutoa sauti ya simu yake.

“Tulipokuwa ndani tulisikia magaidi wakipita hapo wakizungumza kiingera wakiuliza na kiburi”Is anybody here”bado wakiwa wana fyatua marisasi, katika saluni yetu huwezi jua kama mtu yuko ndani sasa walitoka wakaenda.”Alisimulia.

Kulala kwa Tracy si kama kulala kwa mtu ambaye hajawi patwa na tukio kama hili, Tracy akizungumza na radiojambo alisema kuwa haezi lala na amani wala kitu chochote kikianguka anashtuka kwa sababu ya tuko hilo.

Baadaye mama wa yule mteja wangu aliweza kutushauri tusiweze ambia mtu pahali tulipo.

14 riverside drive, dusit

“Nilipokuwa hapo ndani niliona kifo kimefika hivo basi nilianza kumfikiria mtoto wangu nani atatimiza mahitaji yake nani atamchunga atakapokuwa akitoka shule”Aliongezea Tracy.

Kilichomfanya Tracy kusikia vibaya ni vile watu walikuwa wakiongea au kuzungumza mambo mabaya kumuhusu, imepita wiki moja lakini Tracy Wanjiru bado yupo kwenye mshtuko kwa yale yalitokea DusitD2 na ambayo alipitia.

Polisi walipowasili kuwaokoa kutoka mikononi mwa magaidi, hawakuamini kuwa kweli walikuwa ni polisi.Walidhani ni magaidi walikuwa wanawachezea.

Baadaye waliweza kuokolewa na kutolewa katika maeneo hayo.

Pata uhondo kamili.