Connect with us

General News

Tulikosania pesa na mke wangu

Published

on


Bwana Philip alisema alikosana na mkewe bi Norah, miaka miwili iliyopita baada ya ndoa ya miaka kumi na angetaka kupatanishwa naye.

“Tulikosana na yeye kidogo na matanga ikatokea kwao kwani babake alipata ajali. Tulipokosana nilimwambia maneno yameisha na alisema kuwa angetaka kwanza kwenda kwa matanga kabla ajue atakalofanya.

Alipoenda kwao alizima simu na mimi na familia yangu tulishindwa kusafiri hadi matanga kwani hatukuwa na namna ya tutakavyohudhuria. Isitoshe alibeba watoto wote wawili.” Alieleza Philip.

Aliongeza kuwa walikosana baada yake kurudi nyumbani bila fedha kwani anafanya biashara ya bodaboda na pikipiki sio yake. Hivo huwa ngumu kwake kuweza kupata fedha za kutosha wakati mwingine ili amlipe mwenyewe na abakishe zake za matumizi.

Alipopigiwa simu bi Norah, alisema kuwa mumewe alianza kumtesa akiwa na watoto wawili mwaka wa 2009 na hakuacha licha ya wazazi kuingilia kati.

Isitoshe Philip alikuwa na mke wa kando ambaye walikuwa wanaishi pamoja na hakuwa anamshughulikia mkewe.

“Aliuza shamba na nilipokatalia alinipiga. Kunipiga kwake sio kwa mateke wala kiboko yeye ni kuninyonga. Hata huwa anakataa nisiende kanisani wala nisinunue slippers ama mavazi.” Alijieleza bi Norah.

Aliongeza kuwa mumewe alimuacha upweke na mama mkwe bila chakula wala chochote. Isitoshe aliwachiwa majukumu ya kusomesha watoto, kuwatairisha na kuwa hajawahi shughulikia watoto.

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo ili ujue jinsi wawili hao walisuluhisha masaibu yao.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending