Nabii Owuor amekuwa akiishi maisha ya hali ya juu lakini haikuwa kwa jasho lake bali alikuwa akitumia mali ya mwanabiashara maarufu Jayne Muthoni.
Leo ‘Mightiest prophet’ ataweza kueleza kwa kina kuhusu madai hayo.
Nabii Owuor kutuhumiwa kwa kuchukua mali ya billioni 1.5
Owuor ameweza kuitwa katika kituo cha polisi cha Kabete kujibu maswali ya DCI kwa madai kuwa alichukua mali ya Jayne Muthoni.
Jana dadake Muthoni anayefahamika kama Alyce Macharia aliweza kuambia vyombo vya habari kuwa Muthoni ameweza kupelekwa kwa matibabu na kupimwa ili kubaini ni dawa gani alizopewa ili kufanya akili yake iweze kuwa nyonge hivo.
Katika hati zilizotolewa jana zilionyesha kuwa nabii Owuor amekuwa akichukua mamillioni ya pesa kila mwezi kutoka kwa mali ya Jayne Muthoni.
DCI kusukuma mashtaka dhidi ya Henry Rotich
Pia zilionyesha kuwa Owuor ana wafanyakazi, na madereva ambao anawalipa mshahara wa juu kila mwezi. Maafisa, madereva, walinzi na pia wafanyakazi wa nyumba uwa wanalipwa millioni moja kwa mwezi.
Owuor ana madereva wawili yule wa chini akipokea mshahara wa shillingi 70,000 na yule wa juu akipokea shillingi 100,000 kwa mwezi, pia ana walinda lango wawili mmoja akipokea mshahara wa 70,000 kwa mwezi yule mwingineakipokea 100,000.
Pia ana wafanyikazi wa nyumbanii watatu ambao wawili wanalipwa shillingi 52,000 kwa mwezi na mmoja kulipwa 20,000 mabawabu ambao wanamfanyia kazi Owuor huwa wanapokea shillingi 10,000 ya nyumba na kisha kulipwa mshahara wao.
Si wafanya kazi tu pekee wanaishi maisha ya kifahari peke yao kwani nabii huyo aliweza kununua gari sita za dhamana ya juu.
Gari hizo zikiwa sita ni aina ya Mercedes Benz zilizotolewa viwandani kati ya mwaka wa 2004 na 2012 huku Range rover ya millioni 1.4 ikiwa mikononi mwake pia.
Muthoni ambaye ni askofu katika kanisa la nabii huyo alikuwa wakili wa mwendazake George Saitoti ambaye aliweza kumpea Muthoni nusu ya mali yake.
Ni mmoja wa mamillionea ambao waliacha kazi zao na kuanza kusaidia kazi ya nabii Owuor. Maisha ya nabii huyo yalipowekwa wazi DCI aliweza kumuita leo katika kituo cha polisi cha kabete kwa maswali baada ya familia ya Muthoni kudai alinyakua mali ya dada yao.
“Tuliweza kumtumia barua ya kujileta katika kituo cha polisi cha kabete kupitia kwa wakili wake Kimani Watenga.” Alisema polisi wa DCI wa kituo cha kabete.



