Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Vilio na simanzi huku muigizaji maarufu Papa Shirandula akizikwa Busia

Staff
1 min read
Published 20 July 2020

Muigizaji maarufu Charles Bukeko almaarufu Papa Shirandula amezikwa nyumbani kwake Funyula, Kaunti ya Busia.

Shirandula ambaye aliangamizwa na COVID-19 siku ya Jumamosi, Julai 18, alizikwa na maafisa kutoka Wizara ya Afya mwendo wa saa mbili unusu asubuhi.

Habari Nyingine: Bintiye Waziri wa Maji Sicily Kariuki, Wendy Muthoni aaga dunia

Papa Shirandula alizwa nyumbani kwake eneo la Funyula. Picha:CitizenTV.
Source: UGC

Habari Nyingine: Jumatatu Julai 20: Papa Shirandula kuzikwa kesho kijijini Namisi

Hafla hiyo iliandaliwa chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi ambao walihakikisha kuwa sheria za kukabili virusi vya corona zinazingatiwa.

Shirandula alizikwa na maafisa kutoka Wizara ya Afya. Picha:CitizenTV.
Source: UGC

Miongoni mwa wale ambao walihudhuria karamu hiyo fupi ni akiwemo Jacky Nyaminde, almaarafu kama Wilbroda, ambaye ni mmoja wa waigizaji katika kipindi cha Papa Shirandula.

Wilbroda alimuomboleza marehemu kama mtu mkarimu na mwenye upendo ambaye kando na kuwa mwelekezi wake na jirani, alisaidia katika kukuza vipaji vya wasanii wengi chipukizi.

Waombolezaji waliohudhuria mazishi ya Papa Shirandula.Picha: CitizenTV.
Source: UGC

Baba yake Papa Shirandula, Cosmas Bukeko.Picha:CitizenTV.
Source: UGC

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

About the author