Wednesday, 10 June 2026
Kenyan Digest

Viongozi wafokea wabunge kwa kupigana bungeni – Taifa Leo

Staff
1 min read
Published 31 December 2021

Viongozi wafokea wabunge kwa kupigana bungeni

Na TITUS OMINDE

VIONGOZI wa kidini katika maeneo ya Magharibi na Rift Valley wamewataja wabunge kama aibu kwa taifa kufuatia machafuko yaliyoshuhudiwa Bungeni, Jumatano alasiri.

Askofu mkuu wa kanisa la African Divine, John Chabuga alitaja tukio hilo kuwa la kusikitisha huku watu wanaotakiwa kuonyesha heshima na hadhi wakibadilisha bunge kuwa uwanja vita.

“Tulichoona bungeni ni aibu kubwa; bunge lisiwe uwanja wa vita. Wakenya wengi wameamini bunge kuwa mahali pa heshima; tulichoona Jumatano ilikuwa aibu kubwa na ushawishi mbaya kutoka kwa watu tunaowaheshimu,” akasema Askofu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Injili wa Eldoret Askofu Peter Simwa alisema tukio hilo ni ishara tosha kwamba hakuna viongozi waadilifu bungeni.

Askofu Simwa alisema tofauti zinazoshuhudiwa bungeni ni tishio kwa umoja wa nchi, ikikumbukwa kuwa bunge letu limekuwa likichukuliwa kuwa ni kielelezo cha umoja na mahali ambapo sheria nzuri huanzia.

Askofu Sande Mwange wa Kanisa la Jerusalem alisema wabunge walidunisha alitoa heshima yao wakat wakipigana ngumi wakati wa mjadala wa Muswada wenye utata wa Marekebisho ya Vyama vya kisiasa, 2021.

Maoni kama hayo yaliungwa mkono na Askofu Wilson Kurui wa kanisa la Jesus Love Ministries mjini Eldoret

Askofu Kurui alitaja tukio hilo kuwa tabia mbaya kwa vijana ambao wamekuwa wakiliona bunge kama mahali pa heshima.

WANDERI KAMAU: Kupuuza Okwach ndani ya timbo ni kubagua...


About the author