Connect with us

General News

Wahandisi waonya wakazi wa Ruiru dhidi ya kukaribia jumba lililovunjwa – Taifa Leo

Published

on


Wahandisi waonya wakazi wa Ruiru dhidi ya kukaribia jumba lililovunjwa

Na LAWRENCE ONGARO

BODI ya wahandisi wa Kenya, ilizuru eneo ambako jumba moja lilivunjwa na wakati likiporomoka likasababisha maafa mjini Ruiru.

Wakiongozwa na Mhandisi Benjamin Nyawade, walitaka kutoa tahadhari kwa umma ya kwamba ni hatari kukaribia jumba lolote lililoporomoka.

Bw Nyawade, alithibitisha kuwa hivi majuzi watu wawili walifariki katika jumba moja eneo la Bypass mjini Ruiru baada ya jumba hilo kubomolewa.

Halmashauri ya ujenzi wa barabara kuu nchini – KeNHA – ilitoa onyo kuwa jumba hilo lilikuwa limejengwa karibu na barabara kuu ya Thika Superhighway, na kwa hivyo kuna mipango ya kujenga mzunguko katika eneo hilo.

Baadhi ya watu walionekana wakitafuta vyuma.

“Ni hatari kung’oa vyuma hivyo kwa sababu kuna uwezekano ya jumba hilo kuporomoka zaidi jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa binadamu,” alifafanua Bw Nyawade.

Alisema kuwa watu waliopewa jukumu la kubomoa mnjumba makubwa ni sharti waendeshe zoezi hilo kwa makini ili kuzuia maafa kama iliyoshuhudiwa juzi.

“Tumekuwa na vikao kadha na kaunti ya Kiambu ambapo sheria kadha zimepitishwa jinsi ya kujenga majumba makubwa na mbinu za kuhakikisha ni za kudumu,” alifafanua mhandisi huyo.

Alisema kwa sababu jumba hilo limekaribia barabara kuu ya Thika Superhighway, imekuwa ni lazima libomolewe ili mzunguko wa barabara kuwekwa hapo.

Wakati wahandisi hao walipozuru eneo hilo kulikuwa na mkusanyiko wa watu waliokuwa wakitoa mabaki ya vifaa muhimu kama vyuma vya ujenzi na mawe ili wakauze kwa manufaa yao wenyewe.

Wakati huo pia malori kadha yalijazana katika eneo hilo ili kuondoa vifusi vilivyosalia katika eneo hilo.

Hata hivyo Bw Nyawade alitoa tahadhari kwa watu wanaochukua vyuma hivyo wawe makini kuona ya kwamba hawapati majeraha yoyote wakati malori hayo yanapopakia vifusi hivyo ambayo yanaonekana ni vizito.Source link

Comments

comments

Trending