Connect with us

General News

Wajumbe 5,000 wa UDA kumwidhinisha Ruto leo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wajumbe 5,000 wa UDA kumwidhinisha Ruto leo – Taifa Leo

Wajumbe 5,000 wa UDA kumwidhinisha Ruto leo

CHARLES WASONGA na MERCY SIMIYU

ZAIDI ya wajumbe 5,000 wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) wanakongamana leo katika uwanja wa Kasarani, Nairobi kumwidhinisha rasmi Naibu Rais William Ruto kuwa mgombeaji wake wa urais.

Kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi jana, Seneta wa Tharaka Nithi Kithure Kindiki alisema kuwa miongoni mwa wageni wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

“Kando na vinara wenza katika muungano wa Kenya Kwanza, Musalia Mudavadi na Moses Wetang’ula rafiki wetu mwingine ambaye tunamtarajia kufika ni kiongozi wa Narc Kenya Bi Karua. Hii ni kwa sababu Kiongozi wa chama chetu pia amewahi kuwa mgeni katika hafla zao za hadhi kama hii,” akasema.

“Tunawatarajia wageni wengine lakini hatutataja majina yao wakati huu,” Profesa Kindiki akaongeza.

Hafla hiyo inafanyika siku mbili baada ya Dkt Ruto kupigwa msasa na viongozi wa UDA na kuthibitishwa kuwa amehitimu kuwania urais kwa tiketi ya chama chama hicho.

Hii ni baada ya Naibu huyo wa Rais kuwasilisha stakabadhi zake kwa maafisa wa kitaifa wa chama hicho pamoja na risiti ya kuonyesha kuwa alilipa ada ya uteuzi ya Sh1 milioni.

Wapinzani

Hata hivyo, watu wengine wawili ambao pia waliwasilisha maombi ya kutaka kupeperusha bendera ya urais ya chama cha UDA hawakuidhinishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa Jumamosi wiki jana.

Tracy Wanjiru, 23, alikataliwa kwa sababu hakuna na cheti cha shahada, ambayo ni mojawapo ya mahitaji ya kuwania urais.

Wanjiru ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Teknolojia na Kilimo cha Jomo Kenyatta (JKUAT).

Akikubali matokea hayo, msichana huyo alielezea imani yake katika uwezo na ufaafu wa Dkt Ruto kwa wadhifa huo akiahidi kujaribu bahati yake miaka ijayo.

Naye Bw Orina Nyakwama alifeli kuidhinishwa kushindania tiketi ya UDA kuwania urais baada ya kufeli kulipa ada ya uteuzi ya Sh1 milioni iliyohitajika na chama hicho.

Kongamano la leo Jumanne pia linajiri siku chache baada ya muungano wa Azimio la Umoja kumwidhinisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwa mgombeaji wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending