Kaya Godhoma: Wanaosingiziwa uchawi wahangaika mmiliki hifadhi akitaka kuuza shamba
NA MAUREEN ONGALA
MWENYEKITI wa kituo cha kuhifadhi watu wanaosingiziwa kuwa ni wachawi cha Kaya Godhoma katika lokesheni ya Mrima wa Ndege, eneobunge la Ganze Bw Emmanuel Katana ameelezea hofu yake kuhusu usalama wa wazee hao baada ya familia iliyowapa sehemu hiyo kuwaamrisha ama waondoke au wanunue kipande hicho cha ardhi.



