Connect with us

General News

Wawaniaji wapigania Kalonzo Ukambani – Taifa Leo

Published

on


Wawaniaji wapigania Kalonzo Ukambani

Na PIUS MAUNDU

KIONGOZI wa Wiper, Kalonzo Musyoka anakabiliwa na wakati mgumu huku idadi kubwa ya wagombeaji katika eneo la Ukambani waking’ang’ania tiketi ya chama hicho kuwania viti 2022.

Seneta wa zamani wa Kitui, David Musila, ambaye anawania kumng’oa gavana Charity Ngilu katika uchaguzi mkuu ujao, ni miongoni mwa wanasiasa wa hivi punde kurejea Wiper.

Hatua hiyo imepandisha joto la kisiasa katika kaunti hiyo ikizingatiwa kuwa gavana wa zamani wa kaunti hiyo, Julius Malombe na Balozi wa Kenya nchini Uganda pia wanamezea mate tiketi ya Wiper kumshinda Bi Ngilu 2022.

Lakini Gavana Ngilu pia anaonekana kusonga karibu na Bw Musyoka.Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, Mbunge Mwakilishi wa Makueni Rose Museo na aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Cha Mafunzo ya Utabibu Nchini (KMTC) Philip Kaloki wanasaka tiketi ya Wiper ili kurithi kiti cha Profesa Kibwana.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending