Thursday, 12 November 2026
Kenyan Digest

'Fake Uhuru' Walaghai saba kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi 100,000

2 min read
Published

Washukiwa saba waliokuwa wamekamatwa na polisi kwa kumlaghai mwanabiashara wa kampuni ya Sameer na kisha kuiga sauti ya rais, wameachiliwa kwa dhamana ya shillingi 100,000 kila mmoja.

Mahakama ya Nairobi imesema kuwa washukiwa hao saba wako na kesi ya kujibu.

Vile ‘fake Uhuru’ alilaghai mwenyekiti Merali wa kampuni ya Sameer millioni 80

Katika hukumu ya hakimu wa mahakama hiyo Francis Andanyi inasema kuwa walaghai hao,Joseph Waswa, Duncan Muchai, Isaac Wanyonyi, William Simiyu, David Kikuyu, Gilbert Kirunja na Anthony Wafula, watakapopatikana na hatua ya kumlaghai mwana biashara huyo na kuiga sauti ya rais Uhuru Kenyatta wataweza kuenda jela kwa miaka mitatu.

Saba hao waliweza kukana madai hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shillingi 100,000 kwa kila mmoja, lakini jaji huyo alisema kuwa walaghai hao watakuwa wakiripoti katika ofisi ya DCI kila ijumaa kwa muda wa wiki tatu.

Jaji huyo pia aliweza kusema kuwa uchunguzi bado unaendelea, katika mashtaka ambayo yaliweza kusalimishwa mbele ya mahakama Jumanne, walaghai hao walikuwa wameshtakiwa kwa kuiga sauti ya rais wa na kumlaghai mfanyabiashara.

‘Fake president Uhuru’ amlaghai mwanabiashara millioni 80 – Polisi

Mahakama iliweza kukataa kwa washukiwa hao kukaa rumande kwa muda wa siku thelathini.

Katika mashtaka yaliyowasilishwa katika mahakama ilikuwa imeandikwa kwa kiingereza kuwa;

“On January 24 and February 1, 2019 at Prime Bank in Riverside Drive, Nairobi County, the accused jointly conspired with others not before court with intent to defraud, obtained Ksh.10 million from Akif Hamid Butt by falsely pretending that they were in a position to sell to Sameer Africa a piece of land situated in Milimani Area, Nairobi.” Ilisoma mashtaka.

Wasaba hao waliweza kukamatwa na polisi siku ya Jumamosi na wachunguzi wa DCI, kesi hiyo itatajwa machi 11 kwa maelekezo zaidi.

KWINGINEKO: Nikuwa…..

Takribani wagonjwa 53 wameaga dunia katika kaunti ya Taita Taveta tangu mgomo wa wauguzi kuanza.

Nurses’ strike is off, Panyako tells court

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano ya kusitisha mgomo huo, waziri wa afya kaunti hiyo Daniel Makoko amesema wagonjwa hao waliaga dunia kwa kukosa huduma za afya, ambazo zilisambaratika tangu mgomo huo ulipoanza Februari 4.

Hata hivyo amesema idadi hiyo huenda ikawa ya juu zaidi kwani wangonjwa wengi walisalia manyumbani mwao.