Friday, 13 November 2026
Kenyan Digest

Ilikuaje: Mama yangu alibakwa kisha kuuwawa

2 min read
Published

Rose Nyabate ni mwanamke ambaye ameweza kupitia changamoto nyingi na kisha kufaulu maishani, akiongea katika mahojiano na Massawe Japanni, aliweza kusema kuwa alipitia machungu na kuwa katika uchungu kwa kitendo ambacho mama yake aliweza kutendewa.

Ilikuaje: Jacinta Wanjiku aeleza vile alivyoozwa na mama yake

“Niliweza kumpoteza baba yangu nikiwa katika umri mdogo wa miaka miwili.

Mama yangu aliweza kuhama na tukaenda kukaa na yeye mjini Eldoret, baada ya baba yangu kuaga dunia, alianzisha biashara.

Tulikaa kwa muda na mama yangu kisha akaweza kuaga dunia nikiwa na miaka nane.

Mama yangu alikuwa anabeba vyeti vyote,ata hatimiliki alipokuwa akienda katika biashara zake.” Alieleza Rose.

Akiwa katika mahojiano alieleza huku machozi yaki mdondoka na kusema kisa kilicho mkumba mama yake kiliweza kumsumbua kwa sana.

“Siku moja mama aliniambia kuwa atarudi kwa hivyo nisitayarishe chakula. Usiku mama yangu hakuweza kurudi, kesho yake tuliweza kuambiwa kuwa mama yangu amepatikana akiwa amebakwa na kuuwawa.

Si kitendo hicho peke yake wauaji hao waliweza chukua hatimiliki za mashamba, pesa na hata vyeti vyetu vya kuzaliwa.”Nyabate alisimulia.

Baada ya mamake Rose kufariki, ndugu yake alitoroka na kutopatikana kisha wakaja kupatana huku rose akiwa kidato cha nne.

Ilikuaje: Margaret Wajobi asimulia vile aliweza pitia operesheni mara kumi

Alisema pia wakati wa kisa hicho, mama yake aliweza kusikika na mabawabu wa eneo hilo akipiga nduru akitaka usaidizi lakini walipuuza nduru yake.

“Kisa hicho kikitokea mama yangu aliweza kupiga nduru lakini hakuna aliyemsaidia licha ya kusikia nduru yake.

Nimeweza kukuwa na uchungu mwingi moyoni mwangu, mshukiwa aliyekuwa ameshikwa kwa ajili ya mauaji hayo aliachiliwa huru.

Kwa maana ni mimi nilikuwa shahidi mkuu kwa hivyo hawakuweza kuniamini kwani nilikuwa ningali mtoto. Hapo ndipo niliweza kutamani kusomea kazi ya wakili ili siku moja niweze kutetea haki ya mama yangu.” Alizungumza Rose.

Rose ameweza kujaribu kazi kadhaa ata kuwa mcheshi, na kushindikana, hakufa moyo bali aliendelea na masomo na kwa sasa ni mwanabiashara maarufu ambaye amefungua kampuni yake.