Friday, 13 November 2026
Kenyan Digest

Kwanini umdanganye baba yangu ilhali ushaaniua-Beryl Ouma

2 min read
Published

Muda umepita tangu Beryl Ouma auwawe na mume wake Lyko Junior, katika nyumbani kwao kahawa wakati wa mgogoro wa kifamilia waliokuwa nao.

Wapenzi hao walioana mwaka wa 2017, na wamekuwa wakiishi pamoja tangu Lyko aliporudi kutoka Qatar alikokuwa akifanya kazi ya udereva wa ytexi nchini humo.

Unyama! Msichana kubakwa kisha mwili wake kutupiwa asidi

Majirani waliweza kusikia Beryl akipiga nduru bali wakapuuza, ni masaibu ambayo aliweza kupitia ya kuchapwa kabla ya kuweza kufa.

Beryl Ouma

Mwili wa marehemu Beryl ulipofanyiwa upasuaji ripoti ilisema kuwa aliweza kunyongwa akiwa amelala, wakenya wengi waliweza kukasirika kwa sababu majirani waliweza kupuuzilia mbali nduru za Beryl.

Kama wangemsaidia Beryl kutokana na kufanyiwa unyama huo uliosababisha kifo chake.

Katika mahojiano yaliyopita baba yake Beryl Douglas Ouma aliweza kusema Beryl aliweza mtumia jumbe fupi mara tatu na masaa yalikuwa na usiku wa manane.

Jinamizi! One man dies, two seriously injured following a grisly road accident

Alisema pia baada ya kuona ujumbe wa Beryl(please call me) aliweza kumpigia simu ili ajue alivyokuwa akisema bali hakuweza kupokea simu yake.

“Sikuweza kuona jumbe hizo wakati huo huo niliweza kumpigia wakati niliona jumbe hizo, lakini hakuweza kupokea baada ya muda usiokuwa mrefu,

“Mume wake alinipigia na kuniambia kuwa wameweza kukosana,” Alieleza Douglas.

Imekuwa wazi kuwa kabla ya kufariki Beryl aliweza kuongea na baba yake lakini si ana kwa ana baba yake aliweza kusimulia vile alivyosikia sauti yake ya mwisho.

Ni kifo cha kutatanisha kilicho mkumba mwanamke Beryl watu wasijue kilicho mfanya mume wake kumuua kiunyama hivo.

“Niliweza kumpigia mume wake baada ya kumpigia Beryl na kutopokea simu zangu mara kwa mara,

“Niliweza kumsikia msichana wangu tulipokua tunaongea na mume wake alikuwa ana sema kuwa kwanini umdanganye baba yangu ilhali ushaaniua,

‘I caught my hubby pants down 18 times,’ – Narrates Mombasa woman

“Hayo ndiyo maneno ya mwisho ambayo niliweza kusikia msichana wangu akiongea,

“Mume wake aliposikia msichana wangu akiongea na bado tunaongea na yeye kwa simu aliweza kata simu kisha kumpigia tena mara kadhaa hakuweza kupokea simu zangu,” Alisimulia Douglas.