Connect with us

General News

Mume wangu hachukui simu zangu baada ya kupata kazi

Published

on

[ad_1]

Katika kipindi chako ukipendacho cha wanaume waliokimbia majukumu, yaani deadbeat na mtangazaji wako umpendaye Massawe Japanni, mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Kakamega aliyefahamika kama Mary aliweza kupiga simu ili mume wake aweze kupigiwa simu na kupeana sababu za kufanya asiwasaidie watoto wake.

‘Even if I give birth to 500 kids, none of them will be named after my dad’, Angry lady (AUDIO

51697159_172284577099750_3695452994853693993_n(2)

“Mume wangu anaitwa Tony tumeweza kuteseka sana na yeye kwa muda baadaye aliweza kupata kazi Nairobi na kisha kutoka apate kazi hapendi kuja nyumbani,

“Nilimuona mwisho mwaka jana hachukui simu zangu, ata nikimpigia na namba ingine hachukui, na tuko na watoto wawili mmoja anaenda shule na kitinda mimba ana mwaka mmoja na nusu,” Alisimulia Mary.

Alisema kuwa waliweza oana na mume wake kwa miaka mitano sasa aliongezea na kusema kuwa hana kazi licha ya kuwa na watoto wawili ambao wana mahitaji tofauti.

“Sasa hivi sina kazi nikung’ang’ana tu na watoto wangu kwa maana mume wangu alipoenda Nairobi alishikana na mwanamke mwingine,

“Ameacha kusaidia watoto wake,” Alisema Mary.

Mwanamke huyo mwenye machozi alisema kuwa mama wa mume wake yaani mama mkwe huwa analewa chakari na baada ya kulewa mwishowe analeta vurugu katika familia.

PATANISHO: Babangu alitutoroka tukiwa wadogo kwa miaka 11

Nani atakaye chukua jukumu la mwanamume mwingine aliyekataa kutekeleza jukumu lake? ni masaibu ambayo wanawake wengi wanapitia nchini.

Hii ni baada ya kutiwa mimba na mwanaume kisha anatoroka kutekeleza majukumu yake, utawapata wanatembea kama wazuri ilhali mwanamke huyo ana fanya juu chini ili kuahakikisha mtoto au watoto wake wana chakula mavazi na kadhalika.

“Mama yake huwa analewa sana alipokuja jana nyumbani akiwa amelewa aliweza kunirushia vitu vyangu nje huku akiniuliza ninafanya nini katika boma lake,

“Pia aliniambia niweze kutoka kwake na kuwa mtoto wake amepata mke mwingine,” Mary alizungumza.

Mwanaume huyo alipopigiwa simu aliweza kukataa kujibu maswali na kusema kuwa ameshikana, si hayo tu aliweza kumwambia mwanamke huyo aendelee na maisha yake kwa maana yeye ana maisha yake.

Hasira! Wananchi kuchoma gari la polisi kufuatia ajali ya barabara

“Wewe endelea na maisha yako mimi niko na maisha yangu huku,” Alisema Tonny.

Huku mashabiki wa kipindi hicho wakiweza kumshauri mwanamke huyo aende katika wizara ya kutetea haki za watoto.[ad_2]

Source link

Facebook

Trending