Friday, 13 November 2026
Kenyan Digest

Polisi kumuokoa mtoto Tamara aliyekuwa ametekwa nyara

2 min read
Published

Polisi wa DCI waliweza kufanikiwa kumuokoa mtoto Tamara aliyekuwa amedaiwa ametekwa nyara, na kisha kuchukuliwa kutoka mikononi mwa baba yake mzazi.

Kulingana na DCI washukiwa wawili waliweza kukamatwa na polisi kwa kunyakua mtoto huyo eneo la Saika kaunti ya Nairobi.

Wafanya kazi wa JKIA kugoma huku safari za ndege kukatizwa

Washukiwa hao wataweza kupelekwa mahakamani leo ili kujibu mashtaka ya kumuiba mtoto huyo. Aliponyakuliwa kutoka kwa baba yake Timon Makswell, alichukua hatua na kuandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu kisa hicho.

Aliandika huku akitaka haki kutendeka na aweze kurudishiwa mtoto wake ambaye alihaidi mke wake kuwa hatamuacha ateseke.

Ni kisa ambacho kiliweza kuleta tahadhari kwa DCI na kisha kuanza shughuli za kumtafuta mtoto Tamara ili haki iweze kutendeka.

DCI aliweza chukua hatua ya haraka huku akianza uchunguzi wa dharura, ili kumsaidia baba huyo aliyekuwa amenyang’anywa mtoto wa miezi tisa na familia ya mke wake.

‘Long live my dad’: David Rudisha introduces ailing father

Ni kisa ambacho kiliweza kuwaguza wananchi wengi huku wakiweza kuandika heshtegi #JusticeForBabyTamara, kufuatia ujumbe wa baba yake katika mtandao wa Facebook.

Jumatano usiku DCI aliweza kuandika katika mtandao wa kijamii wa twitter maneno yafuatayo;

“Dear #KOT, Detectives from the Child Protection Unit have rescued #BabyTamara & arrested two culprits. The baby is in safe hands & the two suspects are in lawful custody and will be arraigned in court tomorrow. Thank you all for bringing this to our attention,” DCI aliandika.

Tamara

Kulingana na Makswell, mtoto Tamara aliweza kuwachwa mikononi mwake na mama yake kabla ya kuaga dunia Oktoba mwaka jana.

Mwendazake bibi yake aliweza kumuonya kumuacha mtoto wake kwa jamaa zake walios ababisha kifo chake na kutomsaidia, lakini hakuweza timiza ahadi yake wakati dada ya mwendazake mke wake, na mjomba wao kuja na polisi katika nyumba yake na kumchukua mtoto Tamara na kisha kutoweka naye.

Ndege za Nairobi kuenda Tanzania huku wafanyakazi wakipigana na polisi

Makswell alisema kuwa aliweza kukataa na mtoto wake bali polisi hao walimtishia kumfyatua risasi asipopeana Tamara.

Mwanaume huyo alisema kuwa mpwa wa mwendazake mke wake aliweza mjulisha walikuwa wanataka kumtumia Tamara kwa kuomba pesa kutoka kwa wasamaria wema huku wakidai kuwa ni yatima.

“Hivyo ndivyo niliweza kujua kwanini Rena aliweza kusisitiza, nisiweze kupeana mtoto kwa mtu yeyote wa jamaa zao bali niweze kukaa na mtoto wetu.” Alieleza Timon.