Connect with us

General News

“Wakati niliitwa State House ndio nilijua kukalia kiti ya president sio mchezo”

Published

on


Msanii wa nyimbo za injili Bahati alieleza jinsi alijipata matatani mwaka uliopita wakati alipomuamsha rais Uhuru Kenyatta na kukalia kiti chake.

Hilo lilitokea wakati wa kampeini za uchaguzi katika uga wa Kasarani alipokuwa akiwatumbuiza zaidi ya wakenya elfu sitini.

Wengi walimkashifu Bahati kwa tendo hilo huku wengine wakisema iliashiria kuwa amepindua serikali na yeye ndiye rais, hata kama aliketi kwa sekunde kadhaa.

Wakenya waligawanyika kuhusu hilo na wengine walimtetea wakisema hakuwa na nia yoyote mbaya kwani alikuwa katika shughuli ya utumbuizaji.

Bahati kwa upande wake alieleza kuwa hakuona jambo kuu ila maoni ya watu ndio yalifanya ajue kuwa alikuwa amefanya jambo kuu.

Akizungumza na Massawe Japanni, mwimbaji huyo wa ‘Mama’ alisimulia jinsi alishtuka alipoitwa katika ikulu ya rais kufuatia tendo hilo.

Soma usimulizi wake.

By the way nimeona nikama naweza kuwa president some day. Actually nili realize nimekalia hiyo kiti after nimeona kwa news after the story ilianza kuwa big. The moment niliitwa hadi state house ndio nilijua this is serious.

The Kenyan president wanted to meet the ghetto president.

But I think pia ilikuwa a very big sign juu ilikuwa imeanza ku get out of hand and actually that is the best favor that the president ashawahi nifanyia, juu aliifanya ikakaa normal. Juu ilikuwa imeanza kuleta a lot of stories and negativity.

Ni kipi anaeza sema kuwa ni ufanisi mkuu maishani mwake tangia alipoanza usanii?

Of course sitting on the president’s seat and of course when I started my record label, EMB record label, that was a game changer for me because Kenyans hatujakuwa tuki believe in record labels and that is something that is killing the industry.

Tuna need kitu inaweza chukua young people from the streets huko chini watu wako na gifts na wawa support and when I started that, it was a fulfillment in my career and right now I am looking forward to filling Thika stadium on 31st December as EMB Jesus party.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending