Connect with us

General News

Mke wangu huleta wanaume nikiondoka

Published

on


Bwana Joseph alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye walikosana baada ya uchaguzi wa pili, tarehe 26, Oktoba.

“Nilikuwa nimesimamia uchaguzi wa kwanza, kuna mwanadada alinipigia simu kutoka Nairobi akisema kuna kazi lakini ni kama tapeli. Sasa nikasafiri hadi Nairobi lakini IEBC walinitumia ujumbe na ikabidi nirudi kusmamia uchaguzi wa pili. Sasa nikaona nitafika nyumbani mapema nikasimama Nakuru ku watch ball na nikafika nyumbani kitu saa mbili.” Alieleza Joseph.

Wakati nilifika kwa nyumba mke wangu alinishika mkono na kunipeleka nje ya gate akisema kuwa kuna kesi iko kwa chifu na anataka niende nikasuluhishe. Nikalalamika kuwa ni usiku sana na nimechoka, nikakasirika na nikamzaba kofi.

Alikasirika akakimbia na kujifungia kwa nyumba. Sasa jirani yangu akaniambia hatafungua kwani kuna mwanaume amekuwa akiletwa kwangu kila nikitoka. Ndugu zake walimjaribu lakini hakufungua.

Baada ya kwenda training ya IEBC siku iliyofuata nikapata wameondoka na ilibidi nimerudi Nakuru.

Tangia siku hiyo hajawahi muona mkewe lakini huwa wanazungumza kuhusu mambo ya karo ya wanao wawili.

Alipopigiwa simu bi Anne alisema kuwa mumewe anafaa kumtafuta ila sio kumpigia simu kupitia redio.

Hata hivyo, bi Anne alisema ako tayari kurudiana na bwana Joseph akisema amekuwa akingoja hilo.

Pata uhondo kamili.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending