Connect with us

General News

Polisi waanzisha upelelezi baada ya mwili wa mtoto kupatikana huko Taveta

Published

on


Polisi waanzisha upelelezi baada ya mwili wa mtoto kupatikana huko Taveta

Polisi mjini Mwatate kaunti ya Taita Taveta wameanzisha uchunguzi baada ya mwili wa mtoto kupatikana unaelea katika kidimbwi Cha kuogelea katika hoteli moja ya kifahari eneo hilo.

Kulingana na mamake mwendazake Everline Kawa, mwanawe aliondoka siku ya Krismasi na baadaye akatoweka bila kujua alikoenda huku juhudi zao za kumsaka zikigonga mwamba.

Hata hivyo mwili wake umepatikana jana ukielea katika kidimbwi Cha kuogelea katika katika hotel hiyo.

Akithibitisha kisa hicho Mkuu wa polisi mjini Mwatate Monicah Kimani amesema mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi huku wakiendeleza uchunguzi wa kina kutanzua kiini Cha mauti hayo.

Solomon Mwingi Junior

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending