Katika gazeti hili, Waziri wa Masuala ya Kigeni nchini Tanzania, Palamagamba, amewaomba Wakenya kukomesha siasa za ukabila ambazo hushuhudiwa wakati wa uchaguzi.
Waziri huyo aliwambia Wakenya kutengana na siasa za ukabila ili kuzingatia maendeleo na kujenga uchumi.
Palamagamba aliwapongeza Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kwa kuleta utangamano nchini kupitia Jopo Kazi la Maridhiano(BBI).
Kiongozi huyo pia aliwakumbusha wananchi wadhifa wao muhimu ambao wameshikilia katika Kanda ya Afrika Mashariki.
Gazeti la The Standard, Alhamisi, November 28. Picha: Standard Source: UGC
Daily Nation
Kulingana na gazeti hili, baadhi ya Wakenya wameibua hisia mseto kuhusiana na mapendekezo ya kurejeshwa kwa wadhifa wa waziri mkuu huku wakihoji kwamba sio muhimu.
Katika Kaunti ya Kisii, baadhi ya madiwani walisema hatua hiyo ni kuharibu rasilimali ya umma.
Kakamega, Bi. Shillah Chumba ambaye ni mwanabiashara alisema wadhifa huo hautatekeleza masilahi ya Wakenya.
Eneo la Siaya, Daniel Okelo, mkazi wa kijiji cha Olago-Kamkwaya eneo la Bondo alisema kurejeshwa kwa wadhifa huo utasaidia kumaliza mizozo ya uchaguzi.
Gazeti la Daily Nation, Alhamisi, November 28. Picha: Nation Source: UGC
Taifa Leo
Gazeti hili linaripoti kwamba, Makamo wa Rais William Ruto na kiongozi wa Chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi, waliwakashifu wanasiasa ambao wana imani kuwa BBI inapania kuwatunukuu watu fulani nyadhifa kubwa.
Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa ripoti hiyo, Musalia aliwaomba viongozi waliohudhuria kuzingatia zaidi masilahi ya mwananchi wa kawaida.
Mudavadi pia alizungumzia suala la ukosefu wa ajira nchini miongoni mwa vijana.
Ruto, kwa upande wake, alisema BBI haitafaulu endapo wanasiasa wanazingatia masilahi yao kushinda ya Wakenya.
Gazeti la Taifa Leo, Alhamisi, November 28. Picha: Taifa Leo Source: UGC
The Star
Kulingana na gazeti la The Star, mjane wa bwenyenye Tob Cohen anataka kurejeshewa nyumba ya mumewe.
Wairimu, kupitia kwa Wakili wake, alituma ombi la kurejeshewa ufunguo wa nyumba hiyo huku akidai kuwa sio sehemu ya ushahidi.
Hata hivyo, Wakili Cliff Ombetta anayewakilisha familia ya Cohen aliambia mahakama kwamba anahitaji muda kujibu ombi hilo, akisisitiza kwamba mjane huyo sio mmiliki wa nyumba hiyo kulingana na wosia ya Cohen.
Gazeti la The Star, Alhamisi, November 28. Picha: The Star Source: UGC
People Daily
Gazeti hili linaripoti kuwa Rais Uhuru Kenyatta ameamuru kusitishwa kwa makundi ya kisiasa yanayoendesha kampeni za mwaka 2022.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya BBI, Uhuru aliomba makundi chini ya mrengo wa Jubilee; TangaTanga na Kieleweke na makundi ya Inua Mama na Embrace Team kuzima uhasama yao na kusonga mbele.
Rais pia aliwahimiza wanasiasa kujiepeusha na kuleta mgawanyiko nchini kupitia matamshi yao.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269