– Wawili hao wamekuwa wakizozana tangu walipoanza kuishi pamoja
– Mwanawe marehemu ndiye aliyepata mwili huo wakati alipokuwa amemtembelea mamake
– Mshukiwa alitoroka baada ya kutekeleza uhalifu huo
– Maafisa wa polisi wameamzisha msako wa kumkamata mshukiwa huku wakiomba usaidizi kutoka kwa umma
Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Kombok kata ya Ramba eneo la Rachuonyo Mashariki baada ya mjane mwenye umri wa miaka 37, kuliwa na mrithi wake kufuatia mizozo ya kinyumbani.
Mwili wa Margaret Akinyi Otieno ulipatikana umelowa damu baada ya kushambuliwa na mumewe Ademba Ngura.
Mwili huo unaripotiwa kupatikana na mwanawe 7:30 asubuhi, wakati alikuwa amemtenbelea mamake.
Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Rachuonyo Mashariki, Charles Barasa, alisema mwanamke huyo alilemewa na majeraha mabaya ya shingo na kusababisha kifo chake kama ilivyoripoti Nairobi News.
Barasa pia aliongezea kwamba uchunguzi waliofanya ulibaini kuwa mshukiwa alitumia kifaa chenye makali kumtoa uhai mama huyo kabla ya kutoroka.
Mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Rachuonyo Kusini kufanyiwa upasuaji. Source: Depositphotos