Connect with us

General News

Maseneta wanyimwa mlo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Maseneta wanyimwa mlo – Taifa Leo

Maseneta wanyimwa mlo

RICHARD MUNGUTI  NA BRIAN WASUNA

JUHUDI za maseneta kubuni hazina maalumu ambayo wangesimamia katika kaunti ziligonga mwamba Mahakama ya Juu iliposema jana kuwa, jukumu lao ni kuhakikisha kaunti zimesimamiwa vizuri na magavana.

Katika uamuzi wake, mahakama hiyo ya upeo ilitamatisha mvutano kati ya magavana na maseneta kuhusu usimamizi na matumizi ya pesa zinazopelekwa kugharamia maendeleo.

Na wakati huo huo, mahakama hiyo ilikataa kubuniwa kwa hazina ya kaunti ambayo ingesimamiwa na maseneta.

Majaji Martha Koome, Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndungu na William Ouko walisema jukumu kuu la Seneti ni kuhakikisha kaunti zimeendelezwa kwa mujibu wa sheria na zimetumia pesa kama ilivyopitishwa na mabunge ya kaunti.

Jaji Koome na majaji wanne wa mahakama hiyo walisema kubadilishwa kwa sheria hiyo kuwapa maseneta mamlaka ingebuniwa tu kupitia kwa kura ya maoni (referenda).

Pia mahakama ilisema kuwa, haina wajibu wowote kuwatangaza maseneta kuwa wakuu wa magavana.

Pia, walisema maseneta hawana jukumu lolote kuamulia kaunti miradi ya maendeleo itakayopewa kipau mbele.

Jaji Koome na wenzake walisema kubuniwa kwa CDBs na Bunge la Kitaifa ni ukiukaji wa Katiba.

Seneti iliwasilisha rufaa hiyo 2019 ikiomba marekebisho ya sheria za kusimamia serikali za kaunti zikubaliwe na zianze kutekelezwa mara moja.