Connect with us

General News

Korti yagawia mume mali iliyoshikiliwa na mkewe wa zamani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Korti yagawia mume mali iliyoshikiliwa na mkewe wa zamani – Taifa Leo

Korti yagawia mume mali iliyoshikiliwa na mkewe wa zamani

NA BRIAN OCHARO

MWANAMUME aliyeshtaki mkewe na watoto wao wawili akitaka ugavi sawa wa mali, amepata afueni baada ya mahakama kuamrisha apewe sehemu ya mali hizo.

Mwanamume huyo aliyetambuliwa mahakamani kama PMR, aliwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya kifamilia jijini Mombasa baada ya mzozo kuzuka kuhusu mali hizo ambazo ziko katika kaunti za Kilifi na Taita Taveta.

Katika hati zake za mahakama, aliteta kuwa mali anazotaka zifanyiwe ugavi sawa zilipatikana wakiwa katika ndoa na mkewe.

Aliomba kwamba mkewe alazimishwe kutekeleza makubaliano ya awali yaliyowasilishwa mahakamani. Katika makubaliano hayo, mwanamke huyo alitakiwa kutoa stakabadhi zitakazomwezesha kusajili baadhi ya ardhi kwa jina lake.

“Mshtakiwa wa kwanza anaagizzwa kutekeleza na kukabidhi hati zote muhimu za uhamisho ili kuwezesha usajili wa ardhi hizo kwa jina la mlalamishi ndani ya siku 30,” akasema Jaji wa Mahakama ya Familia, Bw John Onyiego.

Jaji huyo pia alielekeza msajili wa ardhi katika Kaunti ya Kilifi kuhakikisha kuwa maagizo hayo yametimizwa bila kukosa.

Pia mahakama hiyo ilimuelekeza msajili wa ardhi kufutilia mbali mahitaji ya kutengeneza upya hati-miliki kuhusiana na ploti hizo.

“Kwa kuzingatia agizo la awali, mahakama imetoa amri kuwa mlalamishi ndiye mmliki wa ardhi hiyo,” akasema.

Jaji Onyiego alitupilia mbali ombi la mwanamke huyo la kutaka kesi iliyowasilishwa na mumewe itupiliwe mbali.

Kupitia maombi yake, mwanamume huyo alilalamikia mahakama kuwa mwanamke huyo amekataa na/au ameshindwa kutekeleza wala kusalimisha nyaraka muhimu kuwezesha uhamisho wa ardhi hizo kwa jina lake kwa mujibu wa makubaliano ya awali.

Aliambia mahakama kuwa huenda akapoteza mkopo ambao tayari umeidhinishwa na benki huku washtakiwa wakiendelea kufurahia matumizi ya mali hizo.

ambazo tayari zimeandikishwa kwa jina lake.

Aidha alisema mkopo uliochukuliwa kwa majina yake na ya mkewe kinakabiliwa na tatizo la kutorejeshwa kwani yeye ndiye anayeshugulikia kuilipia. Alidai biashara ya nyumba za gesti inahujumiwa kwa kushindwa kuendeleza mali ambayo imejengwa.

Mwanamke huyo hata hivyo alisema kuwa masuala yaliyokuwa katika maombi hayo mapya tayari yamesikilizwa na kuamuliwa na mahakama na amri kutolewa.

“Maagizo yaliyoombwa katika ombi hili hayaendani na amri ya mwisho ya mahakama iliyotolewa hapo awali,” alisema, na kuiomba mahakama kutupilia mbali ombi hilo.

Mwanamume huyo alikuwa amewasilisha kesi hiyo mwaka wa 2018 akitaka kugawiwa mali kadhaa zinazodaiwa zilipatikana wakiwa katika ndoa.

Lakini kabla ya kesi hiyo kuendelea, wahusika walikubaliana kwa ridhaa kusuluhisha mzozo huo bila kesi hiyo kusikilizwa kikamilifu.

Makubaliano hayo yalipitishwa kama amri ya mahakama. Idhini hiyo ilielezea jinsi mali zingegawanywa na pia ilimtaka mwanamume huyo aondoe mahakamani kesi ya talaka aliyowasilisha dhidi ya mkewe.

Idhini hiyo pia ilionyesha kuwa walikuwa wamesameheana na wangeanza tena kuishi pamoja kama hapo awali.

Wawili hao pia walikubaliana kuwa mali zote zitashikiliwa kwa pamoja na kuwa ndoa yao iendelee kama hapo awali.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending