Connect with us

General News

Mahangaiko ya Wakenya walio nchini Ukraine – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mahangaiko ya Wakenya walio nchini Ukraine – Taifa Leo

Mahangaiko ya Wakenya walio nchini Ukraine

NA WANDERI KAMAU

RAIA wa Kenya nchini Ukraine wanaojaribu kutoroka mashambulio ya Urusi wameeleza kukabiliwa na matatizo makubwa wanapojaribu kukimbilia usalama wao katika mataifa jirani.

Wakenya hao, wengi wao wakiwa wanafunzi ni miongoni mwa wengine kutoka mataifa kama Tanzania, Nigeria, India na Sudan.

Mwanafunzi Mkenya, Stephanie Iman, alisema maelfu ya watu waliokwama nchini humo wanajaribu kufanya lolote wawezalo kupata chakula na kukimbilia usalama.

Iman, ambaye ni mwanafunzi wa mawasiliano katika Chuo cha Kitaifa cha Kharkiv, alisema ijapokuwa watu wengi wanatorokea nchini Poland, haijakuwa rahisi hata kidogo.

“Tunaishi kwa neema ya Mungu ijapokuwa tuna imani ya kuungana na jamaa zetu,” akasema. Jana, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kenya ilisema jumla ya Wakenya 201 ni miongoni mwa watu waliokwama nchini humo, ijapokuwa wote wako salama.

Kati yao, 183 ni wanafunzi huku 18 wakiwa raia wa kawaida.Wizara ilisema inashirikiana na ubalozi wa Kenya nchini Poland kuhakikisha wamepata usaidizi wa kutosha.Katika taarifa, wizara ilisema Kenya imezungumza na nchi jirani na Ukraine kuwaruhusu Wakenya kutumia mipaka yao kutafuta maeneo salama na kurejea makwao.

“Wakenya wameshauriwa kufanya mipango kuhamia katika maeneo salama ijapokuwa serikali inashauriana na nchi mbalimbali kuwaruhusu kuingia bila vikwazo vya usafiri. Hili ni baada ya baadhi ya Wakenya kukwama katika maeneo ya mipakani baada ya kuzuiwa kuingia katika baadhi ya mataifa,” ikaeleza wizara.

Ijumaa iliyopita, Mwakilishi wa Kike wa Kilifi, Zulekha Hassan, aliishinikiza wizara hiyo kutoa taarifa kuhusu hali ya Wakenya waliokwama katika nchi hiyo.