Connect with us

General News

Bishop wa Githurai aliunganisha mke wangu na jamaa mwingine

Published

on


PATANISHO: Bishop wa Githurai aliunganisha mke wangu na jamaa mwingine

Mzee alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe ambaye anaamini alitoweka na Bishop wa kanisa lao.

Kulingana naye, Bishop alimfanyia mpango ili amnyang’anye mke kisha amzuie kuingia kanisani. Lakini anaamini kuwa Bishop alifanya kazi ya kumuunganisha mke wake na jamaa mwingine.

Soma usimulizi wake.

Mahali tulikuwa tunaenda kanisa Githurai, mimi na familia yangu, kumbe wakati tukienda bishop alikuwa ana connect bibi yangu na mshirika wa kanisa ambaye ananijua na anajua mke wangu vizuri.

Sasa baadaye on 20th August last year, bibi yangu alifika saa tano usiku akiwa ametoka kanisani akapata nikiwa nimefunga nyumba. Vile alibisha sikuskia na kesho yake akaenda kwa chifu apewe barua ya kuachana. Kumbe ni kitu walikuwa wamepanga kwani sikuwa nimemkosea.

Mamake akaitwa kwa chifu ili washughulikie hayo maneno. Bishop naye akanipigia simu akanieleza niendee watoto wangu huko nyumbani na nikifika nimpigie simu aongee na mama ya bibi yangu, kufanya hivyo bishop akamwambia kuwa nipatiwe watoto na wasiwahi kanyaga hilo boma tena.

Sasa nikasafiri nao hadi Nairobi kwa miezi miwili bila bibi, baada ya shule kufunguliwa mke wangu akawachukua na hadi wa leo sijawahi waona. Na nikiuliza habari ya hao watoto wao hunitishia kwani walisema kuwa nilitishia kuchoma kanisa.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending