Connect with us

General News

Chakula cha msaada chaporwa kutoka kwa lori lililoanguka Roysambu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Chakula cha msaada chaporwa kutoka kwa lori lililoanguka Roysambu – Taifa Leo

Chakula cha msaada chaporwa kutoka kwa lori lililoanguka Roysambu

NA SAMMY WAWERU

NAFAKA za thamani ya Sh4.7 milioni ziliporwa Jumanne baada ya lori lililokuwa likizisafirisha kuanguka eneo la Roysambu, barabara kuu ya Thika Superhighway.

Wakazi na wapita njia waligeuza ajali kuwa fursa ya ‘kubeba’ mchele na maharagwe.

Inasemekana chakula hicho kilikuwa cha msaada, na ambacho hadi wakati wa kuchapisha taarifa hii haikuwa imebainika kilikuwa kikipelekwa wapi.

Wahudumu wa bodaboda walisafirisha magunia yaliyokuwa na nafaka hizo, yenye nembo ya GoK.

Machapisho vilevile yaliandikwa, “not for sale”, ishara kuwa chakula hicho kilikuwa cha msaada.

Aidha, lori hilo lilikuwa katika leni ya kasi, barabara ya kuelekea Thika.

“Chakula kilichokuwa kwenye lori kilikuwa chenye thamani zaidi ya Sh4.7 milioni,” akasema mwanamume aliyejitambulisha kwa jina moja tu – Bw Muhamed – na ambaye ni mmoja wa wahudumu waliokuwa wakisindikiza chakula hicho.

Wizi wa nafaka hiyo ulitekelezwa kabla maafisa wa polisi kuwasili kushika doria ya usalama.

Baadhi ya bodaboda zinazodaiwa kushiriki usafirishaji zilitwaliwa.

Hakuna chakula kilichosalia kwenye trela iliyoanguka, Muhamad akidai dereva alipoteza mwelekeo baada ya kukanganywa na gari lililokuwa mbele.

Mchele na maharagwe yaliyomwagika yalitakapaa barabarani na kwenye mitaro ya majitaka.

Mchele na maharagwe yaliyomwagika yalitakapaa barabarani na kwenye mitaro ya majitaka. PICHA | SAMMY WAWERU

Hata ingawa maafisa wa trafiki waliofika walisusia kuzungunza na vyombo vya habari, walisema mkasa huo “ulikuwa ajali kama zinazoshuhudiwa barabarani”.

Imekuwa mazoea ya Wakenya gari lenye mizigo linapoanguka kuipora.

“Ni ishara kuwa wananchi wana njaa, ikizingatiwa kuwa gharama ya maisha imepanda mara dufu,” mmoja wa walioshuhudia akaambia Taifa Leo.

Baadhi ya kaunti hususan zilizoko maeneo kame zaidi zinaendelea kung’atwa na makali ya njaa, na huenda lori hilo lilikuwa likisafirisha chakula cha msaada hadi maeneo hayo.

Zaidi ya kaunti 20 zimeathirika kutokana na baa la njaa, kufuatia ukame unaoendelea kushuhudiwa.

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO limeorodhesha Kenya kati ya nchi tatu katika Pembe ya Afrika zilizolemewa na makali ya ukame.