Connect with us

General News

Mawakili washinikiza sheria ya talaka irekebishwe ili kurahisisha utaratibu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mawakili washinikiza sheria ya talaka irekebishwe ili kurahisisha utaratibu – Taifa Leo

Mawakili washinikiza sheria ya talaka irekebishwe ili kurahisisha utaratibu

NA RICHARD MUNGUTI

KUNDI la mawakili limewasilisha kesi katika mahakama kuu ikiomba sheria ya kupeana talaka irekebishwe na kurahisishwa ili kuepuka maafa yanayochipuka kwenye mchakato huo.

Katika kesi iliyowasilishwa na kampuni ya mawakili ya Copler Attorneys & Consultants jana Jumatatu, inaomba korti iamuru wanandoa wawe wakiwasilisha cheti cha makubaliano kwamba watatengana kisha mahakama inatoa agizo waachane.

Nakala ya cheti hicho cha makubaliano ya kutengana baina ya mume na mke itakuwa ikiwasilishwa katika Mahakama Kuu na nakala nyingine kupelekwa kwa Msajili wa Masuala ya Ndoa ili ndoa ifutiliwe mbali.

Korti imeombwa ishurutishe Mwanasheria Mkuu na Bunge la Kitaifa kufanyia mabadiliko Sheria Nambari 4 ya 2014 kuhusu talaka ili kuepusha familia fedheha, aibu na mizozo inayozuka wanapong’ang’ania mali.

Kampuni hiyo ya mawakili inasema sheria ya sasa ya kutenganisha wanandoa huwasababisha kupata aibu wakitoa ushahidi mahakamani na kuchafuliana majina katika jitihada za kulimbikiziana lawama.

Mbali na wanadoa kukejeliana, watoto wao pia hufedheheka na kukosewa heshima na wazazi wao wanapotusiana mahakamani.

Mahakama imeelezwa kuwa utaratibu unaofuatwa kwa sasa unakera na kuchokesha.

Mahakama imeombwa isikawie kusikiza kesi hiyo kwa vile waathiriwa ni maelfu ya wanandoa ambao hawataki kusema hadharani kwa kuogopa aibu.