Connect with us

General News

Sekta ya utalii yajiandaa Pasaka ikikaribia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sekta ya utalii yajiandaa Pasaka ikikaribia – Taifa Leo

Sekta ya utalii yajiandaa Pasaka ikikaribia

NA WINNIE ATIENO

WADAU wa sekta ya utalii Pwani wameanza kuweka mikakati ya kutafuta faida wakati wa sikukuu za Pasaka.

Wadau hao walikutana Jumapili kujadili mipango mipya ambayo wanaweza kutumia, baada ya mipango ya awali iliyolenga watalii kutoka Ukraine kupata pigo kufuatia vita vya Urusi nchini humo.

Mwenyekiti wa muungano wa vyama vya utalii Pwani, Bw Victor Shitakha alisema idadi kubwa ya wageni waliotarajiwa kutoka nchi hiyo na mataifa mengine ya Ulaya wamefutilia mbali safari zao kwa vile hatima ya vita vinavyoendelea haijulikani.

“Baadhi ya watalii kutoka bara la Ulaya ambao walikuwa wasafiri nchini wamesitisha mipango yao wakisema wanaangalia namna mambo yanavyokwenda wasije Kenya kukwama,” akasema Bw Shitakha.

Bw Shitakha alisema kwa sasa hoteli za Pwani zimejaa kwa asilimia 40 pekee lakini wanatumai kuvuna wakati wa sherehe za Pasaka mwezi ujao.

“Kwa sasa tunategemea mikutano ya serikali, lakini watalii wamepungua sana,” aliongeza.

Afisa wa utalii katika kaunti ya Mombasa Bi Asha Abdi alisema idara yake pia inashiriki kutafuta namna ya kufufua utalii wa kimataifa ili waekezaji wavune wakati wa Pasaka.

Mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa mahoteli, Dkt Sam Ikwaye, alisema uchaguzi mkuu wa Agosti 9, pia umeanza kuleta taharuki miongoni mwa wadau wa utalii kutokana na kuongezeka kwa joto la kisiasa.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending