Biwi la simanzi limetanda katika mtaa wa mauko mjini Busia baada ya mabaki ya mwili wa mtoto wa miaka sita aliyetoweka juma moja lililopita kupatikana kwa shimo la maji.
Mabaki ya mtoto huyo msichana yalikuwa ndani ya gunia huku kichwa kikiwa kimetolewa yaligunduliwa na mchungaji mmoja wa ng’ombe.
Polisi kumuokoa mtoto Tamara aliyekuwa ametekwa nyara
Hellen Barasa alisema mwanawe Anita Barasa alionekana mara ya mwisho na mwanaume juma moja lililopita kabla ya kupatikana ameaga.
Tukio hilo liliweza kuwaacha wananchi wa eneo hilo wakiwa wameshtuka na kupigwa na butwaa.
Hellen alisimulia.
Nyasi ilikuwa imekuwa sana katika eneo hilo kwenye mabaki hayo yalikuwa yametupwa ungeenda hapo haungeona mwili wowote. Hii ni baada ya mchungaji wa ng’ombe kupigwa na harufu mbaya ikitokea eneo hilo, alienda kuangalia na kisha kupata mabaki hayo.
Baada ya mchungaji huyo kukaribia aliweza kuona mwili wa mtoto wangu, na hapo ndipo habari hizo zilienea na kisha zikatufikia.
Wakati ambao mtoto wangu alitoweka alikuwa ametoka shule akakuja, akala chakula na mchana na kisha akaenda kucheza, kabla ya mwanaume kuja na kumdanganya anaenda kumnunulia peremende.
Mvulana wangu aliweza kumfuata mwanaume huyo akilia bali alimwambia aweze kurudi akimuahidi kuwa anaenda na dada yake kumununuliwa peremende ndio aweze kuletea kila mmoja wao.” Alieleza Hellen.
Hellen aliongeza akisema “Mvulana wangu alipowaambiwa watu kuhusu mwanaume huyo hawakuchukulia kama jambo la maana.
Rest well: Sad day for Kenyan sports as David Rudisha’s dad Daniel Rudisha passes on
Walijua ni jambo la maana wakati mvulana wangu aliyekuwa ameenda kuchota maji aliweza kuja na kuanza kumtafuta dada yake.
Mwanaume huyo alikua anatembea na ujasiri mkubwa akiwa na msichana wangu, kwa hivyo watu walifikiria kuwa ni baba yake, baada ya kutoka maombi kanisani jirani yangu aliweza niambia kuwa kuna mwili umepatikana niende nikaone.
Nilienda kuona na nikapata ni mtoto wangu, nilijua ni yeye kwa sababu ya miguu na mikono. Mwili wake ulikuwa umetenganishwa na kichwa, na mwili ulikuwa umeanza kunuka.
Akimaliza kuongea alisema kuwa hakuwa na ugomvi na mtu yeyote na hawajui kama kisa hicho kilikuwa kimepangwa.



