Angalau wafanyakazi waliokuwa wana uhusiana na United Nations waliweza kuaga dunia baada ya ajali ya ndege ya ET302 iliotokea jumapili asubuhi.
Wingu jeusi ili weza kukumba nchi ya kenya kwa kuwapoteza watu 32 katika ajali hiyo, ajali hiyo ilitokea tu baada ya dakika sita baada ya ndege hiyo kung’oa nanga katika uwanja wa ndege wa Addis Ababa.
32 Kenyans among the dead-Ethiopian Airlines releases passenger manifest
Wenye mamalaka walisema kuwa ndege hiyo iliyokuwa na abiria 157 iliweza kuanguka ilipokuwa ikiwaleta abiria hao mjini Nairobi katika kongamano la UN iliyokuwa inapaswa kuanza hivi leo.
“Dalili za mwanzo zilionyesha kuwa wafanyakazi 19 wanaohusiana na UN waliweza kufariki katika ajali hiyo.” Alisema Antonio Vitorino mkuu wa (International Organization for Migration).
Kauli kutoka kwa UN ilisema kuwa (World Food Programme) Iliweza kuwapoteza wafanyakazi 7, miongoni mwa waliofariki wanaohusiana na UN ni Anne Feigl aliyekuwa anafanyia shirika la jumbe katika nchi ya Sudan.
SAD: Former FKF official Hussein Swaleh among those died in Ethiopia plane crash
Catherine ambaye ni kuu katika agendi hiyo ya misheni hiyo aliweza kumkumbuka Anne kama aliyekuwa anajulikana kwa sana na pia aliyekuwa anapenda kazi yake na mchangamfu.
RIP: All 157 passengers aboard crashed Ethiopian Airlines plane are dead
Wakati huo huo mwelekezi wa WFP (World Food Programe ) David Beasley aliyethibitisha kuwa wafanyakazi wake saba wamefariki alisema,
“Tunapo omboleza wenzetu wa WFP, pia tuweze kukumbuka kuwa walikuwa wamejitolea kutembea ulimwengu mzima, na kufanya kazi mbali na familia na jamaa zao,
“Ili kusaidia ulimwengu kuishi maisha mema.” Alizungumza David.
Watu kutoka katika mataifa 35 waliweza kupoteza maisha yao na hakuna ata mmoja aliyenusurika, huku nchi ya Kenya ikiwa na watu wengi ambao walifariki.
Hadi sasa kisa cha ajali hiyo hakijabainiwa ijapokuwa hali ya anga ilikuwa mzuri, baada ya muda mfupi ndege hiyo iliweza kuanguka katika eneo la Bishoftu.
Katibu mkuu wa UN Antonio aliweza kutuma rambirambi zake na kuwa na uzuni mwingi kwa ajili ya jinamizi hilo la ajali, lililofanya wafanyakaza wa UN kupoteza maisha yao.
“Natuma rambirambi zangu kwa familia, marafiki wa waathiriwa, na pia familia za wafanyakazi wa UN waliofariki kupitia mkasa huo,
“Pia kwa serikali ya Ethiopia nawananchi wa nchi hiyo.” Kauli ilisoma.
Alisema pia UN inawasiliana na wenye mamlaka kutoka nchini Ethiopia ili kuwajulisha familia ya wafanyakazi wa UN walioathirika katika ajali hiyo.



