Monday, 16 November 2026
Kenyan Digest

Za mwizi ni 40! Shuhudia jinsi mtaalamu wa kuiba nyama alivyonaswa akisafirisha bidhaa yake ▷ Kenya News

1 min read
Published

Katika hali ngumu ya maisha kila mtu hutafuta jinsi ya kujikakamua kwa njia yoyote ile almradi afike nyumbani angalau na kibaba cha unga.

Lakini bwana mmoja ameibuka mshindi kwa mbinu yake ya pekee ya kusaka posho.

Habari Nyingine: Mama amsahau mtoto, alazimu ndege kurudi uwanjani kumchukua

Picha kutoka video ya jamaa aliyenaswa akiwa amejifunga nyama kifuani. Picha: UGC
Source: UGC

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Ajali ya ndege Ethiopia: Nabii Cosmos Affran alitabiri kuhusu ajali hiyo Februari, 2019

Katika video ambayo TUKO.co.ke imeitizama na ambayo sasa inasambaa kwa kasi mtandaoni, jamaa mmoja amewashtua Wakenya baada ya kunaswa na wanaosadikiwa kuwa polisi akiwa amejifunga mapande mawili ya nyama.

Video hiyo iliyochapishwa Twitter na Sigh @DumeSiugh, jamaa aliyejifunga shuka la Maasai kiunoni na 'jacket' zito na viatu vya plastiki, anaonekana akiamrishwa kulivua jacket lake na watu ambao huenda ndio walioinasa video hiyo.

Habari Nyingine: Ethiopian Airline: Mkenya asimulia alivyowapoteza wanafamilia 5 katika ajali ya ndege

Jamaa huyo anasumbuka kulivua jaketi lake lakini sinema hiyo inachacha wakati mapande ya nyama ya mbuzi aliyojifunga yanapochomozea na kuwafanya polisi kucheka.

Kulingana na video hiyo, huenda hii ndio mbinu ya wizi wa kisasa ambao wezi wa mifugo wameanza kuitumia katika kusafirishia bidhaa za wizi.

Hata hivyo TUKO.co.ke haiwezi kuthibitisha kikamilifu ni wapi alipotoka jamaa huyo na ni maafisa wa kituo kipi waliomkamata.

Lakini mwisho wa siku arobaini zake zilifika na sasa huenda akihitajika kuwataja wenzake katika mtandao wa biashara hiyo ambayo huenda si ya karibuni.

Habari Nyingine: Mama amsahau mtoto, alazimu ndege kurudi uwanjani kumchukua

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke