“Asante Sanaa….Mheshimiwa DC Tandahimba Nakuombea Mungu Nikukute Katika Madalaka Ili Tuisongeshe Tandahimba Mbali Zaidi ….!!!!! Yani Sitamani Upate Uhamisho Ili Kwapamoja Tuitumikie Tandahimba Kuanzia Mwaka 2020 Inshallah..,” aliandika Harmonize.
Ujumbe huo uliwafurahisha wafuasi wake ambao waliahidi kumuunga mkono mbunge wao mtarajiwa.
Harmonize aliwashangaza wengi baada ya kutengana na kiongozi wake wa zamani Diamond Platinumz.
Hatimaye alifuta mchoro wake wa tatto ambayo alikuwa amechora kwenye mkono wake wakati alikuwa anaanza taaluma yake ya muziki
Harmonize, mnamo Jumapili, Desema 8, alipachika picha yake akiwa ameketi na kuanika mchoro mpya wa tatto ambayo awali ilikuwa sura ya Diamond.
Hatua ya Harmonize iliwaduwaza wengi ambao hawakuwa na fahamu kuwa wakati mmoja angechukua mwelekeo huo hususan baada ya kuthibitisha katika mahojiano kadhaa kuwa kutengana kwao kulikuwa kwa kuelewana.