Connect with us

General News

Juventus wapepeta Sampdoria na kukalia vizuri katika nafasi ya nne Serie A – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Juventus wapepeta Sampdoria na kukalia vizuri katika nafasi ya nne Serie A – Taifa Leo

Juventus wapepeta Sampdoria na kukalia vizuri katika nafasi ya nne Serie A

Na MASHIRIKA

ALVARO Morata alipachika wavuni mabao mawili na kusaidia waajiri wake Juventus kucharza Sampdoria 3-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Jumamosi.

Ushindi huo uliwezesha Juventus kukalia vizuri katika nafasi ya nne jedwalini na kuweka hai matumaini ya kujitwalia taji la Serie A muhula huu wa 2021-22.

Maya Yoshida wa Sampdoria alijifunga katika dakika ya 23 na kuwaweka Juventus uongozini kabla ya penalti ya Morata katika dakika ya 34 kuwapa masogora wa kocha Massimiliano Allegri uhakika wa kutamalaki mchuano.

Japo kipa Wojciech Szczesny wa Juventus alipangua penalti ya Antonio Candreva, Sampdoria walifutiwa machozi na Abdelhamid Sabiri dakika sita kabla ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo kupulizwa. Morata alifungia Juventus bao la tatu kunako dakika ya 88.

Juventus kwa sasa wamejizolea alama 56 kutokana na mechi 29 huku pengo la pointi saba pekee likiwatenganisha na viongozi wa jedwali AC Milan waliotandika Empoli 1-0. Ni pengo la alama tisa ambalo sasa linatamalaki kati ya Juventus na nambari tano Atalanta ambao wamesakata michuano 27 pekee.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO