Connect with us

General News

Matiang’i aamuru wahudumu wa bodaboda wajiunge na vyama vya ushirika – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Matiang’i aamuru wahudumu wa bodaboda wajiunge na vyama vya ushirika – Taifa Leo

Matiang’i aamuru wahudumu wa bodaboda wajiunge na vyama vya ushirika

NA WINNIE ONYANDO

WAHUDUMU wote wa bodaboda watahitajika kujisajili kupitia mfumo wa kidijitali ili kupata leseni mpya iliyoidhinishwa na Mamlaka ya Kitaifa ya Usafiri na Usalama Barabarani (NTSA).

Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i alisema, hatua hiyo ndiyo itaikomboa sekta hiyo na kuwaondoa wahalifu wanaojificha miongoni mwao.

Alisema zaidi ya Wakenya 2.5 milioni wanategemea sekta hiyo na hakuna haja wahangaishwe na polisi kwa sababu ya wahalifu wanaoweza kukomeshwa.

Kadhalika, alitoa wito kwa wahudumu wote wa bodaboda wajisajili ili kuepuka adhabu ya serikali.

Akizungumza jana na viongozi wa wahudumu wa bodaboda kutoka kaunti mbalimbali jijini Nairobi, Dkt Matiang’i pia alisema kuna haja wahudumu katika sekta hiyo wajiunge na vikundi mbalimbali vya ushirika ili kurahisisha kazi ya serikali hasa katika utoaji wa misaada na huduma mbalimbali zinazolenga kuwafaidi.

“Wahalifu ambao wamejificha miongoni mwa wahudumu wa bodaboda watakamatwa wote. Ikiwa kila mmoja atajisajili na kujinga na Sacco, basi tutasafisha sekta hiyo,” akasema Dkt Matiang’i.

Kwa upande mwingine, alitoa wito kwa wasimamizi katika sekta hiyo kushirikiana na serikali na hata kuwahamasisha wenzao kuhusu sheria za trafiki ili kupunguza ajali na vifo miongoni mwao.

Kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake, Dkt Matiang’i alisema tayari serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuwalinda akina mama walio katika sekta hiyo.Kwa kipindi cha miezi miwili, usajili utafanywa bure bila malipo.

Ili kujisajili, mamlaka hiyo inahitaji kitambulisho, nambari ya simu, anakotoka mhudumu wa bodaboda na nambari ya siri ya KRA.

Leseni hizo zitakuwa na habari zote kuhusu mhudumu wa bodaboda ili kurahisisha kazi ya serikali, hasa wakati wa msako wa wahalifu ama ajali inapotokea.

Wahudumu wa bodaboda 200,000 watakaojisajili wa kwanza watapata mafunzo ya bure kuhusu sheria za trafiki kutoka Huduma ya Kitaifa ya Vijana (NYS).