Connect with us

General News

Fowadi Jermain Defoe astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Fowadi Jermain Defoe astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39 – Taifa Leo

Fowadi Jermain Defoe astaafu soka akiwa na umri wa miaka 39

Na MASHIRIKA

NYOTA wa zamani wa West Ham United, Tottenham Hotspur na Rangers, Jermain Defoe, amestaafu soka katika umri wa miaka 39 akivalia jezi za Sunderland nchini Uingereza.

Defoe aliyejiunga na Sunderland mnamo Februari 2022 ameangika daluga zake baada ya kupachika wavuni mabao 304 kutokana na mechi 762 za ligi mbalimbali. Aidha, alifungia timu ya taifa ya Uingereza magoli 20 kutokana na mechi 57.

Defoe ambaye amesakata soka ya kitaaluma kwa miaka 22, aliwahi pia kuchezea Portsmouth, Bournemouth na Toronto katika Major League Soccer (MLS) nchini Canada.

“Nilijitosa katika ulingo wa soka kitaaluma nikiwa na umri wa miaka 17 pekee mnamo 1999,” akasema Defoe aliyefunga jumla ya mabao 162 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Hadi kustaafu kwake, anashikilia nafasi ya tisa kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote katika kipute cha EPL tangu 1992-93. Aidha, anashikilia nafasi ya 15 kwenye orodha ya wanasoka ambao wamewajibishwa mara nyingi zaidi katika kipute hicho ambacho amekinogesha mara 496.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO