Connect with us

General News

Beki Ben White ajiondoa kambini mwa Uingereza kwa sababu ya jeraha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Beki Ben White ajiondoa kambini mwa Uingereza kwa sababu ya jeraha – Taifa Leo

Beki Ben White ajiondoa kambini mwa Uingereza kwa sababu ya jeraha

Na MASHIRIKA

BEKI Ben White wa Arsenal amejiondoa kambini mwa timu ya taifa ya Uingereza kutokana na jeraha na sasa amerejea kambini mwa waajiri wake kutibiwa uwanjani Emirates.

Nyota huyo wa zamani wa Brighton mwenye umri wa miaka 24 alitiwa katika kikosi cha awali cha wanasoka 27 watakaotegemewa na kocha Gareth Southgate kwenye michuano mitatu ijayo ya Uefa Nations League dhidi ya Hungary, Ujerumani na Italia.

Trent Alexander-Arnold ataungana na wenzake kambini mwa Uingereza mnamo Mei 31, 2022 baada ya kuchezea Liverpool dhidi ya Real Madrid kwenye fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Wanasoka wengine wanaotazamiwa kambini mwa Uingereza kufikia mwisho wa Mei 31 ni Raheem Sterling wa Manchester City, Kieran Trippier wa Newcastle United na James Ward-Prowse wa Southampton.

Uingereza watavaana na Hungary ugenini mnamo Juni 4, 2022 kabla ya kumenyana na Ujerumani kisha Italia baadaye.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO