Connect with us

General News

Embu: Pasta ajutia kuwachokoza walevi ▷ Kenya News

Published

on

[ad_1]

Pasta kutoka eneo la Matendeni alijipata pabaya baada ya kujaribu kuvuruga kikao cha walevi.

Duru za kuaminika zinaarifu kwamba, mhubiri huyo alifika mahali hapo ambapo polo hao walikuwa wakipiga mtindi akitaka kuhubiri.

Habari Nyingine: Sababu zinazotajwa kuhusu kuteketeza miili ya waliofariki dunia badala ya kuzika

Kulingana na Taifa Leo, pasta huyo alipowasili hapo alianza kuwatawanya huku akiwaita majina machafu machafu.

“Ondokeni hapa mara moja. Nataka kuwahubiria watu hapa na siwezi kufanya hivyo ikiwa hamtaondoka,” pasta huyo alisikika akiwaambia walevi.

Alipoona anapuuzwa na walevi hao, alianza kuwashambulia kwa cheche za maneno.

Habari Nyingine: Kalonzo: 2022 sitakubali kumuunga yeyote mkono

Hata hivyo, walevi hao waliamua kumgeukia na wakaanza kumzomea.

“Hapa si kanisa pa kuhubiri nenda mahali pengine na uache kutuchokoza,” jamaa mmoja alimpasha pasta.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko



[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending