– Wawili hao walikuwa wanampeleka mshukiwa aliyekuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi bangi hiyo
– Bangi hiyo ilikuwa imefichwa ndani ya chupa ya chai
Watu wawili walikamatwa Alhamisi, Juni 3 na misokoto 17 ya bangi ambayo walikuwa wanampelekea mshukiwa aliyekuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kirinyaga.
Washukiwa hao wa kike Frida Njeri na Doreen Wambui wenye umri wa miaka 18 na 22 mtawalia walikuwa wanamtembelea James Murithi ambaye alikamatwa kwa ulanguzi wa bangi.
Wasichana hao walikuwa wameficha bhangi hiyo ndani ya chupa ya chai. Picha: Citizen Digital. Source: UGC
Maafisa wa polisi waliozungumza na Citizen Digital walisema wawili hao walikamatwa kabla ya kumpa mshukiwa chupa cha chai ambayo walitumia kubeba dawa hizo.
Polisi waliwashurutisha kuifungua chupa hiyo ambayo misokoto ya bangi ilikuwa imefichwa chini yake.
Wawili hao walikuwa wanampeleka mshukiwa aliyekuwa amezuiliwa katika kituo cha polisi bangi hiyo. Picha Source: UGC
Mmoja wa washukiwa hao aliwaambia polisi Muriithi aliwaambia hakuwa akijihisi mzima kwa kuwa hakuwa amevuta bangi kwa zaidi ya siku mbili.
“Alituambia tutumie ujanja huo na kumpenyezea bangi hiyo kizuizini kwani hakuwa akijihisi mzima baada ya kuikosa kwa siku mbili,” Wambu aliwaambia polisi.