Magazeti ya Jumatatu, Novemba 25, yameripoti pakubwa kuhusu ripoti ya Jopo la Maridhiano maarufu BBI ambayo inatazamiwa kukabithiwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani  Raila Odinga.
Kisa cha hivi majuzi cha maporomoko ya ardhi eneo la  Pokot Magharibi ambapo watu 40 walipoteza maisha yao pia ni taarifa nyingine iliyopewa uzito.
Habari Nyingine: Polisi wawili wafumaniwa na kamanda wao wakimeza hongo 
Magazeti ya Kenya Jumatatu, Novemba 25.
Source: UGC
 
Habari Nyingine: Jowie afunguka kwa mara ya kwanza kuhusu maisha yake gerezani 
Daily Nation
Kulingana na gazeti hili, Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga wanatazamiwa kuandaa kongomano la Jopo Kazi la Maridhiano maarufu BBI siku ya Jumatano, Novemba 27.
Rais amewaalika mawakilishi 100 kutoka kaunti zote 47 kwa mkutano wa kushauriana utakaoandaliwa katika ukumbi wa  Bomas.
Kamati ya BBI itamkabithi rasmi Uhuru na Odinga ripoti hiyo kesho Jumanne, Novemba 26.
Hii ni kufuatia hali ya sintofahamu na hamu katika nyanja ya siasa huku kundi laTangaTanga likisema litaunga mkono ripoti hiyo endapo inawashirikisha kila mmoja.
Gazeti la Daily Nation. Jumatatu, Novemba 25. Picha: Nation
Source: UGC
 
The Standard
Katika gazeti hili baadhi ya familia 40 kutoka kaunti ya Murang’a zimeagizwa kuhamia maeneo salama kwa sababu ya tishio la maporomoko ya ardhi .
Shirika la Msalaba Mwekundu limewaomba wakazi wanaoishi maeneo ya Kangema na Mathioya kuhama kwani maeneo hayo yanashukiwa kushuhudia maporomoko ya ardhi.
Mkurugenzi wa Idara ya hali ya hewa kaunti ya Murang’a, Paul Murage ametambua mahali 88 katika kaunti ndogo za  Mathioya, Kahuro, Kangema na Kigumo kuwa na nyufa.
Haya yanakujia baada ya maafa ya Pokot Magharibi ambapo zaidi ya watu 40 walizikwa wakiwa hai mnamo Ijumaa, Novemba 22.
Gazeti la The Standard Jumatatu, Novemba 25. Picha: Standard
Source: UGC
 
The Star
Gazeti hili linaripoti kuwa kaunti 15 zitakosa kupokea pesa za ugavi wa mapato kwa kushindwa kulipa madeni.
Kaunti hizo ni pamoja na Narok, Machakos, Nairobi, Vihiga Isiolo, Tana River, Migori Tharaka Nithi na Kiambu
Hazina ya Kitaifa ilisema kaunti hizo zilishindwa kufuata maagizo ya Baraza Shirikishi la Bajeti na Masuala ya Uchumi (IBEC) linaloongozwa na Naibu wa Rais William Ruto.
Gazeti la The Star,Jumatatu, Novemba 25. Picha: Star.
Source: UGC