Mwanamke afungwa miaka 12 baada ya kumdhulumu kingono mtoto wa miaka 5
Mwanamke mmoja mwenye umri wa maka 21 amehukumiwa kifungo Cha miaka 12 gerezani na mahakama ya Voi kaunti ya Taita Taveta baada ya kupatikana na hatia ya kumdhulumu kingono msichana wa miaka 5.
Mwanamke huyo kutoka kijiji cha Mwakingali mjini Voi alikiri mashtaka mbele ya hakimu Ann Karemi.
Inadaiwa kuwa kati ya mwezi Disemba mwaka jana na tarehe 10 mwezi huu, alitumia vidole kumdhulumu kingono mtoto huyo kinyume cha sheria (Sexual assault contrary to section 5) na hivyo kumsababishia majeraha katika sehemu zake za siri.
Hakimu Karemi anasema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ulionyesha wazi kwamba mshukiwa alitenda kitendo hicho mara kadha.



