Connect with us

General News

Seneta Omanga aahidi kumpa Kwamboka 100K za kumshtaki Maraga

Published

on

– Omanga alisema yuko tayari kumlipia fedha za kutafuta wakili ili kumshtaki Jaji Mkuu Maraga

– Alisema Maraga ni mzee wa kuheshimiwa na atampa Kwamboka KSh 100K ili kutafuta haki akidhibitisha madai yake

– Kwamboka alizua kizaazaa mahakamani baada ya kudai amekuwa mchumba wa siri wa Jaji Mkuu

Seneta mteule wa Jubilee Millicent Omanga ameahidi kuwa atamlipia ada ya mawakili binti aliyedai kuachiwa majukumu ya ulezi na Jaji Mkuu David Maraga.

Omanga alimtaka binti huyo kumdhibitishia kuwa ni kweli walikuwa na uhusiano na Maraga na kujaliwa mtoto.

Seneta Omanga aahidi kumlipia Kwamboka ada ya mawakili akidhibitisha uhusiano na Maraga

Jaji Mkuu David Maraga alidaiwa kushiriki uhusiano wa kimapenzi ulioishia mtoto msichana kuzaliwa.

Mary Kwamboka Onyancha alichipuka Jumanne, Juni 30, na kudai amekuwa kwenye uhusiano na Jaji Mkuu kwa miezi sita.

Alisema uhusiano wao uliishia mtoto wa kike na Maraga ametelekeza majukumu yake kama baba.

Omanga, kupitia kwa mtandao wake wa Twitter, alionekana kushuku madai ya Kwamboka na kusema iwapo ni kweli, basi atampa 100K.

Seneta Omanga aahidi kumlipia Kwamboka ada ya mawakili akidhibitisha uhusiano na Maraga

Seneta Millicent Omanga aliahidi kumlipia Mary Kwamboka ada ya mawakili akidhibitisha uhusiano wake na Jaji Maraga. Picha: Millicent Omanga
Source: Facebook

“Niko tayari kuku[pa 100K kulipia huduma za wakili na uchunguzi wa DNA kama utanidhibitishia kuhusu uhusiano wenu na Maraga,” alisema Omanga.

Seneta huyo alisema Jaji Mkuu ni mtu wa kuheshimiwa kwenye kanisa lake la sabato na hafai kupakwa tope.

Seneta Omanga aahidi kumlipia Kwamboka ada ya mawakili akidhibitisha uhusiano na Maraga

Mary Kwamboka ambaye alidai amekuwa kwenye uhusiano na Jaji Mkuu Willy Mutunga.

Maraga, kupitia kwa mawakili wake, alipuuza madai hayo akisema hiyo ni njama ya kumpaka tope.

“Mwanamke huyo anatumiwa na wale ambao wanataka kumtimua Maraga kutoka afisini. Kumekuwa na presha nyingi Maraga ajiondoe ama astaafu kabla ya kukamilika kwa kipindi chake ambacho kitakamilika Januari 12, 2021,” wakili wake Danstan Omari alisema.

Comments

comments

Facebook

Trending