Tishio la Kaburu Trump la kuatimua wahamiaji walioishi Marekani kwa miongo kadhaa, waweza kuwa si utani tu. Wakati huu anapoizindua nia yake ya kugombea kiti cha urais wa Marekani kwa mara ya pili, ni vema kukumbuka kwamba kuna baadhi ya mamillioni ya wazungu wenye “shingo nyekundu” ambao, liwalo lolote lile, sharti watampigia kura mwenda wazimu huyu. Kutokana na tishio hili, ningewaomba wenzetu haswa Wakenya kulitafakari hatua hio na kujipanga kwa vyovyote vile. Njia moja wazo za kujipanga ni:
1. Hama na ubadirishe makaazi, anwani na nambari yako ya simu haraka iwezekanavyo. Ukifanya hivyo utawachanganya na kuhitilafu habari aliokuwa nayo kukuhusu wewe.
2. Kama tayari ulikuwa umenunua nyumba, iweke sokoni haraka iwekenavyo ili iuzwe na kuzipeperusha dola hizo Jamhuri. Usipofanya hivyo, miaka hio yote umelipia nyumba hio itapotelea mbali, na mabenki yatasherehekea kwani wataiuza tena kwa faida kubwa.
3. Ukiwa ulikuwa umenunua gari nzuri, ichape bei, kisha ununue kidubweshe mkebe wa gari cha kukufisha kazi na kwingineko, na ambapo likitendeka lolote, hutapoteza jasho yako.
4. Wakikudaka, kama itawezekana, wacha walipie nauli ya ndege ya kukurudisha makwenu.
5. Kuanzia wakati pumbavu Trump alipotangaza hivyo, kuwa Mkenya mpweke, na kaa mbali na Wakenya kwani wengi wao, hawajawahi kupendezwa na bidii yako ambayo imewapita wao.
6. Toa pesa zako zote zilizo kwenye benki na kuzifurusha akaunti yako Jamhuri, na pia toa peasa zilizo katika kadi zako zote za Bank of Amerika, American Express, Visa, MasterCard, Credit Unions,
7. Hakikisha kwamba unauwezo wa kutoa pesa kutoka kwa akaunti iingiako mshahara wako popote ulimwenguni, ili likitendeka, waweza kuzitoa kutoka akaunti yako ya Equity, COOp bank, Family bank, ABC, Commercial Bank of Africa, Barclays, Standard Bank, na kadharika. Usiwe na kadi ya checking account ambayo inakuruhusu tu utoe pesa zako ukiwa Marekani pekee.
8. Anza kujitayarisha kifikra, kimawazo, kifedha ili likitendeka na ujione Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, hutashikwa na butaa au mgutuko wa roho.
9. Ichukue jamaa yako kwenya mlo wa jioni hasaa watoto, mahali Wendy’s, Friday, Buffee na pengineko kisha uwaeleze ukweli uliopo, hatua kwa hatua.
10. Usiruhusu jamaa yako huko Kenya kujua kilicho kibetini au akaunti yako Kenya. Na ikiwezekana, kama kwenu ni Muranga, enenda Nakuru, Nyahururu, Naivasha au Kajiado. Kama kwenu ni Kakamega au Kisumu, enenda Nairobi, au kwingineko. Chukua muda kutulia ili kuhimili vishindo vya nchi mpya, bila kuchanganya na jamaa yako au marafiki.
11. Tafuta Mkenya unaemuamini akuwekee cheti cha pasipoti, kipande na vyeti vyako vyoko vya shule.
12. Muombe Maulana mbaguzi Trump apigwe na radi au mhemuko na mshutuko wa misuli, isiwe ikawa vile alivyopanga.
13. Uza chochote kilicho cha dhamani kwako, au tafuta rafiki umwaminie kukihofadhi kwa niaba yako. Kisha kaa turi kama maji ya mtungi.
Na waombea neema na ushindi katika pilka pilka hizi za muovu shetani. Amina.