Katika mahojiano na shirika la BBC, msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres , Stephane Dujarric, alikitaja kitendo hicho kama cha kusikitisha na kukera.
“Tumeshtushwa na kushangazwa na kile kinachoonekana katika video hii,”
”Tabia kama hiyo ni kinyume na chochote kile tunachokiamini”, alisema Dujarric.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alikitaja kitendo hicho kama cha kusikitisha. Picha:UGC. Source: UGC
Kulingana na UN, wale waliohusika wanaaminika kuwa maafisa wa kulinda amani nchini Israel na wanakaribia kutambuliwa.
Umoja wa Mataifa una sheria kali dhidi ya tabia za ngono miongoni mwa wafanyakazi wake na wanaweza kuadhibiwa iwapo watakiuka sheria hiyo.
Kando na hayo muungano huo umekuwa ukichunguzwa kufuatia madai ya dhuluma za ngono ambayo imekuwa ikiwahusisha maafisa wake na wasichana wachanga.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aliahidi kukabiliana na shutuma za utovu wa nidhamu wa kingono katika muungano huo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.