Connect with us

General News

Sausage rolls – KenyanDigest

Published

on

Idadi ya walaji :4

Viungo

  • vikombe vya unga wa ngano 3
  • kijiko cha hamira 1/4
  • sukari vijiko vikubwa 3
  • chumvi kijiko cha chai 1/4
  • kikombe cha mafuta ya uto 1/2
  • yai
  • maziwa kikombe 1 1/2
  • soseji 8
Sausage rolls – Taifa Leo
Soseji nane. Picha/ Mishi Gongo

Jinsi ya kutayarisha

Chukua unga wa ngano, hamira, sukari, chumvi na mafuta ya uto kisha changanya.

Ongeza yai na maziwa katika mchanganyiko na ukande hadi unga ulainike.

Tengeneza donge kisha uache uumuke.

Unga na viungo kadhaa. Picha/ Mishi Gongo

Ukishaumuka kata unga kidogo kisha tengeneza kama rolls au minyororo.

Lingalinga mnyororo kwa soseji kisha panga kwa treya ya kuoka.

Rolls au minyororo ya unga ikiwa imezungushwa kuzingira soseji kabla ya kuoka. Picha/ Mishi Gongo

Oka kwa muda wa dakika 10.

Unaweza ukapakua ukala chakula hiki huku ukinywa ama sharubati ya machungwa au chai.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending