Connect with us

General News

Mhubiri na mwandishi Robert Burale akutwa na virusi vya COVID-19

Published

on

[ad_1]

Mhubiri na mwandishi maarufu wa vitabu Robert Burale amethibitisha kuwa amepatikana na virusi vya COVID-19

Kupitia ujumbe alouandika kwenye mtandao wa Facebook, Burale alisema alijihisi kushindwa kupumua na alipofika katika hospitali ya Nairobi, alifanyiwa vipimo na kupatikana na virsi hivyo.

Kwa sasa mhubiri huyo ametengwa ila anahofia afya ya bintiye ambaye wanaishi pamoja.

“Nilipatikana na virusi vya corona, saa 24 baada ya kufanyiwa vipimo, daktari aliingia kwenye chumba nilichokuwa nimetengwa, sikufurahia matokeo kwa kusema ukweli, hata hivyo naamini Mungu yupo,” Burale alisema.

Burale pia alithibitisha kuwa ugonjwa wa corona upo na watu walioambukizwa wanaumia kupindukia.

” Bado ninashangaa, niliingizwa katika chumba kilichohifadhiwa wagonjwa wa COVID-19, nikama haya yote ni matukio ambayo mimi huona kwenye sinema,nilikaribishwa na daktari ambaye alinitia moyo, nilishtuka kwa kusema ukweli lakini najipa moyo kwa sasa,”Burale aliongezea.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos



[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending